Rais wa Jamhuri ya muungano wa
Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisisitiza jambo mbele ya Viongozi wa
Serikali na wafanyakazi wa Bohari ya Dawa (MSD) wakati akizindua magari
mapya 181 ya Bohari ya Dawa (MSD) yatayotumika kusambaza Dawa na Vifaa
tiba,
………………
NA WAMJW-DAR ES SALAAM.
ILI kufikia katika uchumi wa kati
kwa kutumia sekta ya viwanda Serikali inatakiwa kujikita katika
kuimarisha sekta ya afya kwa watanzania ili kuwa na rasilimali watu
wenye afya njema
kwa ajili ya kuleta mafanikio hayo kupitia viwanda.
Hayo yamesemwa na Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli wakati wa uzinduzi wa
magari 181 ya kusambazia dawa uliofanyika leo katika Bohari Kuu ya Dawa
ya Taifa (MSD) jijini Dar es salaam.
“Tunatakiwa kuwekeza kwenye uchumi
wa Viwanda ili tufikie uchumi wa kati hivyo ni lazima tuwekeze kwenye
sekta ya afya kwa kiwango kikubwa ili kuwa na wananchi wenye afya njema
tayari kutumikia viwanda vyetu kwa muda wote” alisema Rais Magufuli.
Aidha Rais Magufuli amesema kuwa
Tanzania inatakiwa kujijengea viwanda vya dawa na vifaa tiba hapa nchini
ili fedha zinazotumika kununua bidhaa hizo nje ya nchi zirudi mikononi
kwa watanzania wenyewe pamoja na kutoa ajira kupitia viwanda hivyo.
Mbali na hayo Rais Magufuli
amesema kuwa katika kuimarisha Sekta ya afya Serikali imetenga shilingi
Bilioni 269 za kununua dawa katika bajeti ya mwaka wa fedha 2017/2018
kutoka bilioni 31 katika bajeti ya fedha mwaka 2016/2017.
Kwa upande wake Waziri wa
afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu amesema
kuwa katika kuimarisha Afya ya mama na Mtoto Serikali imepunguza vifo
vitokanavyo na uzazi kwa asilimia 60 kutoka asilimia 20 ya upunguzaji wa
vifo hivyo.
Aidha Waziri Ummy amesema kuwa
fedha zilizotengwa kwa ajili ya dawa zina mgawanyo ikiwemo asilimia 42
zahanati na vituo vya afya ,asilimia 16 zinatumika kwa chanjo za watoto
,asilimia 10.2 zianenda hospitali za wilaya ,asilimia 6.8 zinatumia
hospitali za mikoa ,asilimia 3.4 zinaenda hospitali maalum na asilimia 3
zinatumika kwa ajili ya dawa za saratani.
“Fedha hizo za dawa zipatazo
Shilingi Bilioni 269 asilimia kubwa zinaenda kwenye vijiji na kata
pamoja na zahanati na vituo vya afya na kufanya hali ya upatikanaji wa
dawa kuwa juu mpaka kufikia hivi sasa” alisema Waziri Ummy.
Waziri Ummy amesema kuwa licha ya
kuwa tu kuna upatikanaji dawa wa hali ya juu nchini lakini Serikali
kupitia Wizara ya Afya imetengeneza muongozo wa matibabu kwa ajili na
kuwataka waganga wafawidhi wote nchini kutumia muongozo huo ili kutoa
matibabu sahihi kwa wagonjwa .
Kwa mujibu wa Waziri ummy amesema
kuwa katika kuimarisha sekta ya Afya nchini Serikali imejitahidi
kuongeza huduma za matibabu ya kibingwa kwani hivi sasa katika Hospitali
ya Taifa ya Muhimbili inapandikiza figo pamoja na vifaa vya usikivu kwa
watoto ambapo imepelekea kupunguza rufaa za nje na kuokoa fedha nyingi.
Naye Mkurugenzi wa Bohari Kuu
ya Dawa ya Taifa nchini (MSD) Bw. Laurean Bwanakunu amesema kuwa
wanasambaza dawa za shilingi bilioni 18 kila mwezi na lengo ni kufikia
bilioni 21 kufika mwezi julai mwaka huu.
Aidha Bw. Bwanakunu amesema kuwa
mbali na upatikanaji wa dawa kuongezeka lakini kuna chanagamoto za
maoteo kutoka ngazi ya zahanati kwani wanashindwa kujua mahitaji yao
sahihi ya dawa zinazohitajika kwa mwaka hivyo kufanya MSD kushindwa
kupeleka dawa kwa wakati.
Samabamba na uzinduzi huo wa
magari hayo 181 ya kusambazia dawa na vifaa tiba hapa nchini
yaliyotolewa kwa ushirikiano wa Seikali ya Tanzania pamoja na Mfuko wa
Dunia wa pamoja (Global Fund) pia Mhe. Rais Magufuli alipata kutembelea
maghala ya dawa yaliyopo MSD jijini Dar es salaam.
No comments :
Post a Comment