Waziri wa Kazi, Ajira, Sera,
Bunge, Vijana na wenye ulemavu, Jenista Mhagama akikata utepe kuashiria
uzinduzi wa miundombinu ya usalama barabarani katika shule za Msingi
Mikumi na Mzimuni ikiwa ni mwendelezo wa mpango wa uboreshaji wa usalama
barababarani kwa wanafunzi wa shule za msingi jijini Dar es Salaam
ambao unaratibiwa na shirika la Amend kwa ufadhili wa Mfuko wakampuni ya
Puma Energy na Mfuko wa FIA. Wanaoshuhudia ni pamoja na Mkurugenzi Mkuu
wa Puma Energy Tanzania, Bw Philippe Corsaletti, walimu na maofisa wa
Jeshi la Polisi kikosi cha usalama Barabarani.
Waziri wa Kazi, Ajira, Sera,
Bunge, Vijana na wenye ulemavu, Jenista Mhagama akikabidhi msaada wa
jaketi la usalama barabarani kwa mwanafunzi Nuru ambae ni Muhanga wa
ajali za barabarani. Nuru alilazimika kukaa hospitali kwa kipindi cha
miaka miwili akipatiwa matibabu baada ya kugongwa na gari maeneo jirani
na shule hiyo.
Waziri wa Kazi, Ajira, Sera,
Bunge, Vijana na wenye ulemavu, Jenista Mhagama akishirikiana na
wanafunzi wenye ulemavu kutoka shule ya Gilman Rutihimaba kuimba nyimbo
zenye mafunzo ya usalama barabarani.
Mkurugenzi Mkuu wa Puma Energy Tanzania, Bw Philippe Corsaletti akizungumza kwenye hafla hiyo.
Waziri wa Kazi, Ajira, Sera,
Bunge, Vijana na wenye ulemavu, Jenista Mhagama akiwa kwenye picha ya
pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa Puma Energy Tanzania, Bw Philippe
Corsaletti, walimu na wanafunzi wa shule za Msingi Mikumi na Mzimuni.
Waziri wa Kazi, Ajira, Sera,
Bunge, Vijana na wenye ulemavu, Jenista Mhagama akiwa kwenye picha ya
pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa Puma Energy Tanzania, Bw Philippe
Corsaletti, na maofisa wa shirika la Amend, Jeshi la Polisi kikosi cha
usalama Barabarani, walimu wa shule za Msingi Mikumi na Mzimuni.
Waziri wa Kazi, Ajira, Sera,
Bunge, Vijana na wenye ulemavu, Jenista Mhagama akigagua miundombinu ya
usalama barabarani iliyojengwa kupitia mpango huo. Wengine ni pamoja na
Mkurugenzi Mkuu wa Puma Energy Tanzania, Bw Philippe Corsaletti
No comments :
Post a Comment