Serikali kupitia Programu ya
Miundombinu ya Masoko, Uongezaji Thamani na Huduma za Kifedha vijijini
(MIVARF) imeweza kuinua maisha ya wananchi wa Vijijini katika Wilaya ya
Meru na Mbulu Mkoani Arusha katika kuongeza thamani ya maziwa na kilimo
cha vitunguu saumu.
Akizungumza na wataalamu kutoka
MIVARF Meneja wa Kiwanda cha Maziwa cha The Grand Demam Deo Temba
alisema, tulikuwa tunasindika maziwa lita 300 kwa siku ambayo
yalikuwa
ni maziwa machache kulingana na uhitaji wa wananchi, lakini sasa
tunaweza kusindika maziwa 2500 kwa siku baada ya kupata uwezeshaji
kutoka MIVARF kwa kutujengea chumba cha Baridi yaani Cold Room.
“Tangu kujengwa kwa chumba cha
baridi tumeweza kuongeza bidhaa za maziwa kupitia vikundi 15 ambapo
katika vikundi hivyo vina idadi ya watu 120-150 inayofikia idadi ya watu
2026 wanaoleta maziwa kiwanda”, alibainisha Temba.
Kiwanda cha The Grand
Demam.co.Ltd kimeweza kuwaunganisha wafugaji na kiwanda kwani kiwanda
kinawapatia elimu ya jinsi ukamuaji wa maziwa kwa tija ili waweze kupata
maziwa bora mengi pamoja na ufugaji bora kwa kuwa na mifugo michache na
kutoa maziwa mengi na kuwapa huduma za matibabu kwa mifugo yao.
Mkulima kutoka katika Wilaya ya
Meru Hilda Mroso alieleza kuwa, hapo awali alikuwa akikamua maziwa
mengi lakini alipeleka lita 300 za maziwa katika Kiwanda cha The Grand
Demam kutokana na ukosefu wa mahali pa kuhifadhia, kwa sasa anauwezo wa
kupeleka maziwa lita 800 kwenye Kiwanda hicho kutokana na kuongeza
sehemu ya kuhifadhia maziwa hayo.
Aidha, Programu ya MIVARF pia
imewekiwezesha kiwanda cha Kusindika Vituguu cha Bashay Wilayani Meru
kwa kuwapatia mashine ya kukaushia vitunguu ambapo hapo awali walikuwa
wakikausha vitunguu kwa kutumia jua au Solar Drier iliyokuwa
ikiwachukulia muda wa wiki moja hadi sita kukausha vitunguu hivyo.
Mkulima wa zao la Vitunguu
Boniface John alieleza, kabla ya uwezeshaji wa Programu ya MIVARF
Kiwanda cha Kusindika Vitunguu cha Bashay kilikuwa kinasindika kwa
shida sana na kwa muda mrefu na kusindika vitunguu vichache sana.
“Upatikanaji wa Mshine hii ya
kukaushia vitunguu, imekiwezesha kiwanda chetu kuboresha huduma za
usindikaji kwani mashine inauwezo wa kukausha Tan moja hadi mbili za
Vitunguu saumu kwa masaa nane sawa sawa na gunia 20, hivyo tunaweza
kukausha kwa haraka, na imetusaidia kuongeza wateja kwani tuna kamilisha
oda zetu kwa wakati haya ni maendeleo makubwa sana katika Kijiji chetu
cha Bashay, alisema Mkulima huyo. ”
Kiwanda hicho kwa sasa kinauwezo
wa kuuza bidhaa iliyoongezwa thamani kwa kuuza kitungu saumu kilicho
sagwa yaani unga na rojo ya vitunguu saumu imewasaidia kuuza kwa urahisi
na kujiongezea kipato.
MIVARF; ni Programu ya Miundo
Mbinu ya Masoko na Huduma za Kifedha Vijijini iliyobuniwa na serikali
ya Tanzania kwa kushirikiana na Mfuko wa Kimataifa wa Maendeleo ya
Kilimo yaani (IFAD) na Benki ya Maendeleo ya Afrika (ADB). Lengo kuu la
Mpango huu ni kufanikisha azma ya Serikali ya kupunguza umaskini na
kuongeza kasi ya ukuaji wa uchumi endelevu kwa kuziwesha kaya za
vijijini kujiongeza kipato na usalama wa chakula.
No comments :
Post a Comment