Said Khatib (kulia), ambaye ni Wakala wa Tigo Pesa katika eneo la Mkunazini, Zanzibar akipokea mfano wa hundi ya TSH milioni tano kutoka kwa Afisa Mkuu wa Huduma za Kifedha wa Tigo – Hussein Sayed (wa tatu kulia). Khatib aliibuka mshindi wa pili kitaifa katika promosheni ya mawakala wa Tigo Pesa ambapo Tigo imetoa jumla ya TSH 88 milioni kwa mawakala wake zaidi ya 73,000 nchini walioshiriki katika promosheni hiyo. Wengine katika picha ni Mtaalam wa Masoko wa Tigo Pesa – Restituta Kedmond (wa pili kulia), Meneja wa Maendeleo ya Masoko wa Tigo – Innocent Mosha (wa pili kushoto) na Meneja wa Maendeleo ya Mifumo ya Usambazaji, Katherine Lusenge.
Nane (8) wapata TZS 3 millioni na TZS 2 millioni kila mmoja, huku mamia wengine wakizoa zawadi na bonasi lukuki
Dar es Salaam, 14 Machi, 2018.
Kampuni
inayoongoza kwa huduma za fedha kwa njia ya mtandao, Tigo Tanzania
kupitia huduma yake ya Tigo Pesa leo imewazawadia wakala wake mamilioni
ya pesa kwa utendaji wao mzuri.
Wakala
RBB RBB ya Sinza, Dar es Salaam ilijishindia TZS 10 millioni kutoka
Tigo Pesa, huku Said Khatib wa Mkunazini, Zanzibar akijinyakulia zawadi
ya pili ya TZS 5 millioni katika promosheni iliyohusisha mawakala zaidi
ya 73,000 wa Tigo. ‘Nilishinda zawadi ya kanda katika promosheni
iliyofanyika mwezi Desemba kwa hiyo nafurahi kuwa uwekezaji na juhudi
nilizofanya katika kipindi hiki vimeniwezesha kutangazwa kama mojawapo
wa washindi wa kitaifa,’ Khatib alisema.
Pamoja
na zawadi hizio kwa washindi wa kitaifa, Tigo pia ilitoa zawadi nane za
TSH 3 millioni na TZS 2 millioni kwa mawakala bora kutoka kila kanda
nchini. Pia zawadi za bonasi zilitolewa kwa mawakala wote waliofikia
malengo waliowekewa katika kipindi cha promosheni hiyo.
Mojelwa
Mlinga wa Ukonga, Dar es Salaam aliyeibuka kama wakala bora wa kanda ya
Pwani na kujinyakulia kitita cha TZS 3 milioni alisema kuwa atatumia
hela alizoshinda kuboresha mtaji wake wa biashara. ‘Nilishinda zawadi
ya pili kitaifa katika promosheni iliyofanyika mwezi Desemba na nilikuwa
natarajia kushinda zawadi ya kwanza kitaifa, ila nashukuru kuwa
nimefanikiwa kupata zawadi ya kanda,’ alisema.
Akizungumza
katika hafla ya kukabidhi zawadi kwa washindi iliyofanyika katika ofisi
za Tigo jijini Dar es Salaam, Afisa Mkuu wa Huduma za Kifedha wa Tigo,
Hussein Sayed alisema kuwa lengo kuu la promosheni hiyo ilikuwa ni
kuwadhamini na kuwashukuru mawakala zaidi ya 73,000 wa Tigo Pesa
walioshiriki katika promosheni hiyo kote nchini.
“Ningependa
kuwapongeza mawakala wetu kwa kazi kubw wanayofanya ya kuhakikisha kuwa
huduma za kifedha zinapatikana kwa urahisi kwa watu wote kote nchini,’
alisema.
Tigo Pesa ni huduma ya fedha ya simu za mkononi ya pili kwa ukubwa nchini.
Kampuni
ya Tigo ilianza kutoa huduma nchini Tanzania mwaka 1995 na kwa miaka
mitatu mfululizo ndiyo kampuni ya simu inayokua kwa kasi zaidi nchini.
Kwa sasa Tigo ndio kampuni ya simu za mkononi ya pili kwa ukubwa nchini
inayohudumia wateja zaidi ya 11.6 milioni.
Tigo
ni kampuni inayoongoza kwa mageuzi ya kidigitali nchini na inatoa
huduma bora za kipekee za sauti, SMS na intaneti ya kasi ya juu ya 4G
inayopatikana katika miji 24 nchini kote. Tigo pia inafahamika kwa
promosheni kabambe na ofa bunifu kwa wateja wake.
No comments :
Post a Comment