Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia wakati wa
ufunguzi wa Mkutano wa Halmashauri Kuu ya Shirikisho la Michezo la
Mashirika ya Umma na Makampuni Binafsi Tanzania (SHIMMUTA) uliofanyika
Chuo Kikuu Dodoma (UDOM) Machi 27, 2018 mjini Dodoma.
Wajumbe wakifuatilia kwa makini
hotuba ya Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan wakati wa ufunguzi wa
Mkutano wa Halmashauri Kuu ya Shirikisho la Michezo la Mashirika ya Umma
na Makampuni Binafsi Tanzania (SHIMMUTA) uliofanyika Chuo Kikuu Dodoma
(UDOM) Machi 27, 2018 mjini Dodoma.
Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais
……………….
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan amewataka Viongozi
wa Mashirika ya Umma na Makampuni Binafsi kuwaruhusu wafanyakazi
kushiriki michezo katika maeneo yao ya kazi lakini pia wawaruhusu
wafanyakazi hao kushiriki Michezo ya SHIMMUTA.
Makamu wa Rais ameyasema hayo
wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa Halmashauri Kuu ya Shirikisho la
Michezo la Mashirika ya Umma na Makampuni Binafsi Tanzania (SHIMMUTA)
mjini Dodoma.
Makamu wa Rais amesema michezo ni
muhimu sana kwenye Tanzania ya Viwanda kwani michezo husaidia mwili kuwa
wenye afya bora na utendaji wao wa kazi unakuwa mzuri zaidi.
Makamu wa Rais amesema yeye
alikuwa mwanamichezo mzuri wa mpira wa pete (netball) lakini kwa sasa
anafanya mazoezi kidogo kidogo asubuhi na jioni.
“Najua Umuhimu wa kufanya mazoezi
kwa sababu nikiacha kufanya mazoezi nadorora na katika nafasi hii
ukidorora unadorora mpaka akili na kazi zitakushinda”
Makamu wa Rais aliwasihi Viongozi
wa Michezo kusimamia masuala ya michezo katika maeneo ya kazi na
kuwataka Viongozi wa Taasisi kuweka bajeti ya michezo kwa ajili ya
kushiriki michezo ya SHIMMUTA.
Makamu wa Rais amesema ilani ya uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi ya 2015- 2020 imeleekeza kuendeleza michezo sehemu za kazi.
Aidha Mwenyekiti wa SHIMMUTA Ndugu
Hamis Mkanachi alimpongeza Makamu wa Rais kwa juhudi anazozifanya
katika kukuza michezo nchini.
No comments :
Post a Comment