Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais
TAMISEMI, Mhe. Selemani Jafo (Mb) akimkabidhi moja ya gari la wagonjwa
aina ya Suzuki Maruti, Ashura Nkya ambaye ni Kaimu Mkurugenzi wa
Halmashauri ya wilaya ya Babati katika bandari ya Dar es Salaam jana.
Baadhi ya magari aina ya Suzuki
Maruti ambayo Mhe. Rais Dkt. John Pombe Joseph Magufuli aliamuru
yagawiwe katika Mamlaka za Serikali za Mitaa ili kuhudumia Sekta ya Afya
nchini.
……………………………………………………………………………………
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais,
Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI), Selemani Jafo,
ameendesha zoezi la kugawa magari 50 ya wagonjwa aina ya Suzuki Maruti
(Ambulances) kwa Mamlaka za Serikali za Mitaa nchini Jijini Dar es
Salaam.
Magari hayo ambayo awali Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli
aliagiza yafanyiwe utaratibu wa kisheria wa kiforodha na
yagawanywe
kwenye Mamlaka za Serikali za Mitaa ili yatumike kwa kuwahudumia
wananchi katika vituo mbalimbali vya afya nchini.
“Hii ni agenda ya Mhe. Rais ya
kutaka kuhakikisha watanzania wanapata huduma bora, ambulance hizi ulaji
wake wa mafuta ni mdogo sana na zitatusaidia katika halmashauri
nyingi,”amesema Jafo.
Aidha, Mhe. Jafo amemshukuru sana
Rais wa John Magufuli kwa kuonyesha mapenzi makubwa lakini pia
amependezwa na Watumishi wa Wizara, Mikoa na Halmashauri
zote kuweza kuhudhuria hafla hiyo muhimu iliyofanyika bandarini Jijini Dar es Salaam.
Naye Naibu Katibu Mkuu
anayeshughulikia Afya Ofisi ya Rais TAMISEMI, Dkt. Zainabu Chaula
amemshukuru Waziri wa Nchi TAMISEMI na Waheshimiwa Wabunge wote kwa
utendaji wao na kuwataka wabunge kuwa na lugha ya ufahamu mmoja ili
kuboresha utendaji Serikalini.
“Kwa niaba ya watendaji
nawashukuru sana waheshimiwa Wabunge, nilitamani tutembee pamoja kwa
maana ya kuwa na uelewa wa pamoja na ndio maana Mhe.Waziri amewakabidhi
wabunge magari nao watukabidhi sisi,”Amesema
Charles Kichere Kamishna Mkuu wa
Mapato Tanzania, amesema awali magari hayo aliyaona Mhe. Rais alipofanya
ziara bandarini na kwamba magari hayo yalikuwa yameteleekezwa na
mmiliki wake kutofahamika na ndipo rai, aliagiza kufuata utaratibu wa
forodha na kuyataifisha magari hayo na kasha yagawiwe kwenye Mamlaka za
Serikali za Mitaa nchini.
Kwa upande wake Mhe. Prof Norman
Sigalla King, Mbunge wa Makete, amemshukuru Mhe. Rais kwa kutoa
ambulance hizo kwa ajili ya kuimarisha huduma za mama wajawazito.
“kwanza nitoe shukrani za pekee
kabisa kwa kupewa ambulance kwa ajili ya wilaya yangu ya Makete
nakumbuka niliomba kwa ajili ya tarafa za Ukutama, Matamba, Magomba,
Tulongwa na Niwaho”amsema.
Amebainisha umbali wa kata ya
Ukutama hadi Makete mjini ni kilomita 70 na hivyo itawanusuru wakina
mama dhidi ya vifo vya uzazi visivyotarajiwa.
Kaimu Mkurugenzi Halmashauri ya
Wilaya Kigoma, Hakimu Ndatama amemshukuru Mhe. Rais kwa kuwapatia
ambulance ambayo itaokoa vifo vya akina mama na watoto kwa kiasi
kikubwa.
No comments :
Post a Comment