Mashine mbalimbali za kusaga na kuboa mahindi zilizobuniwa na kutengenezwa na SIDO Iringa.
Moja ya tenki la kuchuja asali,
tenki hili limebuniwa na wajasiriamali wa TEJO NATURAL HONEY na
kutengezwa na Karakana ya SIDO Iringa.
Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya
Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Ludovick Nduhiye akisalimiana na
waheshimiwa wabunge mara baada ya kuwasili katika ofisi za SIDO ili
kupokea taarifa iliyoandaliwa na SIDO Mkoa wa Iringa.
Makamu mwenyekiti wa kamati ya
Viwanda, Biashara na Mazingira Mhe. Innocent Bashunga (mb) akizungumza
wakati wa kupokea taarifa ya SIDO Iringa, pembeni ni Naibu Waziri Wizara
ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mhe. Mhandisi Stella Manyanya (mb)
Mkuu wa Karakana SIDO Iringa
Mhandisi Nestory H. Ngoromela akitoa maelezo kwa kamati ya kudumu ya
Bunge Viwanda, Biashara na Mazingira.
Viti na bidhaa mbalimbali za mbao zilizo buniwa na kutengenezwa na wajasiriamali walio chini ya SIDO Iringa.
Naibu Waziri Wizara ya Viwanda,
Biashara na Uwekezaji, Mhe. Injinia Stella Manyanya akiangalia bidhaa
mbalimbali za wajasiriamali walio chini ya SIDO Iringa.
Baadhi ya wabunge wa kamati ya ya
kudumu ya bunge Viwanda, Biashara na Mazingira wakiangalia bidhaa
mbalimbali zinazotengezwa na wajasiriamali walio chini ya SIDO Iringa.
………………..
Kamati ya kudumu ya Bunge Viwanda,
Biashara na Mazingira yakutana na Mhe. Naibu Waziri wa Wizara ya
Viwanda, Biashara na Uwekezaji na ku[pokea taarifa ya SIDO Iringa.
katika taarifa yao SIDO
wameeleza shughuli mbalimbali wanazofanya hasa katika kusaidia
wajasiriamali na wafanyabiashara kwa kuwapa elimu, mikopo yenye riba
nafuu na ujuzi.
Baada ya kupokea taarifa hiyo
kamati ya bunge ikiongozwa na makamu mwenyekiti Mhe. Innocent Bashunga
(mb) ilitembelea eneo la SIDO Iringa na kujionea shughuli mbalimbali za
uzalishaji zinazofanywa kiwandani hapo na kutembelea kiwanda cha Darsh
ambacho pia walisaidiwa katika ubunifu wa baadhi ya mashine kiwandani
hapo lakini pia SIDO ndio waliohusika katika ushawishi wa uanzishwaji wa
kiwanda hiko ili kusaidia wakulima wa nyanya.
Kamati ya bunge imeishauri
Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji kufanya juhudi kubwa kusaidia
shirika hili la SIDO kwani ndio nguzo pekee kuelekea uchumi wa Viwanda,
hivyo ni lazima kusaidiwa kupata teknolojia za kisasa ili kusaidia
wajasiriamali kuzalisha bidhaa bora na zenye ushindani katika masoko ya
kimataifa.
No comments :
Post a Comment