Friday, March 23, 2018

KAMATENI HATA MAGARI KWA KAMPUNI ZISIZOLIPA MIRABAHA-BITEKO

Naibu Waziri madini Dotto Biteko(katikati mwenye kizibao chekundu) akikagua  bidhaa zinazozalishwa na mgodi wa mawe wa Udbhav international Ltd  uliopo  kijiji cha Ntyuka manispaa ya  Dodoma alipotembelea jana katika ziara yake ya kawaida  ya kikazi.
 Mmiliki wa mgodi wa mawe wa China Dragon Internation .co.Ltd Sist Mganga (wa kwanza kushoto) akimpa maelezo naibu waziri wa madini Dotto Biteko (wa pili toka kushoto) alipotembelea juzi mgodi huo uliopo Kijiji cha Itiso Wilaya ya Chamwino Mkaoni Dodoma

 Naibu Waziri Madini Dotto Biteko(katikati mwenye kizibao chekundu) akikagua mashimo ya mgodi wa machimbo ya madini ya dhahabu katika kijiji cha Nholi Wilaya ya Bahi Mkoani Dodoma alipotembelea jana kwenye ziara yake ya kawaida ya kikazi.

 Naibu Waziri  wa Madini Dotto Biteko akizungumza na wachimbaji wa  mgodi wa machimbo ya madini ya dhahabu katika kijiji cha Nholi Wilaya ya Bahi Mkoani Dodoma alipotembelea jana.

 Naibu Waziri  wa Madini Dotto Biteko akikagua machimbo ya madini ya dhahabu katika kijiji cha Nholi Wilaya ya Bahi.

 Naibu Waziri  wa Madini Dotto Biteko akizungumza na wachimbaji wa  mgodi wa machimbo ya madini ya dhahabu katika kijiji cha Nholi Wilaya ya Bahi Mkoani Dodoma alipotembelea jana.

NAIBU Waziri wa Madini Dotto Biteko ameagiza kukamatwa kwa magari na vitendea kazi kwa kampuni za ujenzi wa barabara zinazodaiwa fedha za mirabaha kwa kuwa zinatakiwa kulipa kwa mujibu wa sheria.
Biteko ametoa agizo hilo baada ya kupewa taarifa na Afisa  madini mkazi wa Dodoma Silimu Mtigile kuhusu madai ya makampuni hayo wakati wa ziara ya siku ya moja
kutembelea migodi ya uchimbaji madini katika mkoa wa huo.
Amesema kampuni yeyote ya ujenzi wa barabara inayodaiwa fedha za mirabaha na serikali haitaruhusiwa kuondoa mitambo yake kwenye eneo kazi hadi itakapolipa.
Ameeleza kuwa kampuni hizo zinapaswa kulipa madeni ya tozo mbalimbali wanazodaiwa na Serikali.
Hata hivyo Biteko amewataka wasimamizi wa serikali katika kukusanya kodi hizo kuwa waaminifu na wasiisababishie serikali hasara kwa kurubuniwa na wadaiwa.
Ameagiza Ofisi ya madini ikutane na wahusika wa madeni hayo ya kodi ya madini katika maeneo yao ya kazi ili kutoa elimu jinsi ya kulipa kodi hizo zinazostahili.
Awali katika taarifa aliyoitoa kwa Naibu Waziri huyo, Afisa madini huyo amesema kuna baadhi ya wakandarasi wa ujenzi wa barabara wanadaiwa deni la mirabaha ya ujenzi  zaidi ya sh. bilioni 1.9 na wameshalipa Sh.milioni 642.5.
Ametaja wakandarasi hao kuwa ni kampuni ya Chico ilikuwa inajenga barabara ya Mayamaya hadi Mela , CRSG ambayo ilijenga barabara ya Mela hadi Bonga, Sinohydro Company ambayo imejenga barabara ya Dodoma mjini hadi Mayamaya na CCCC iliyojenga barabara ya Dodoma hadi Fufu.
Aidha amesema katika mwaka wa fedha wa mwaka 2016/17 madini waliweka malengo ya kukusanya maduhuli ya serikali kiasi cha sh.Bilioni 1.2 ambapo walivuka malengo kwa asilimia 120.34 kwa kukusanya zaidi ya Sh.bilioni 1.4.

No comments :

Post a Comment