Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya
FINCA Microfinance, Tanzania Issa Ngwegwe akizungumzia mafanikio ya
sherehe zake FINCA Microfinance kutimiza miaka 20 ya utendaji wake wa
shughuli za kifedha nchini Tanzania tangu kuanzishwa kwake.
Mwenyekiti wa Bodi ya FINCA
ambaye pia ni Makam wa Rais na Mkurugenzi wa Kanda ya Afrika Mike
Gama-Lobo akizungumza katika mkutano huo.
Rais na Mkurugenzi Mtendaji wa
FINCA Microfinance Holding Company, Andree Simon akiipingeza FINCA
Microfinance kwa kufanya kazi kwa ufanisi wa hali ya juu.
…………………………………………………………………………………..
Banki ya FINCA Microfinance,
miongozi mwa benki maarufu zinazotoa mikopo midogo midogo nchini
Tanzania, kwa mafanikio makubwa wakati ikiwa imefikisha miaka 20 tangu
kuanzishwa kwake hapa Tanzania.
Issa Ngwegwe amesema hayo katika
mkutano na waandishi wa habari kwenye hoteli ya Serena jijini Dar es
salaam wakati akiwaeleza waandishi wa habari kuhusu sherehe za taasisi
hiyo na Mafanikio ya miaka 20 ya FINCA katika kutoa huduma za kifedha
zilizo salama na
kuwezesha wajasiriamali wadogo nchini Tanzania ambapo
mgeni rasmi katika hafla hiyo anatarajiwa kuwa Makamu wa Rais wa
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Mheshimiwa Samia Sululu Hassan
Amesema sherehe hizo
zinatarajiwa kuhudhuriwa na zaidi ya wageni 300 ambao ni Bodi ya
Wakurugenzi wa FINCA, Uongozi wa FINCA, wafanyakazi na viongozi wa juu
kutoka katika mtandao wa FINCA pamoja na wageni waalikwa mbalimbali.
Akielezea kuhusu hali ya
ukopeshaji ya FINCA, Ngwegwe amesema: “Tangu FINCA ilipoanzishwa mwaka
1998, imeweza kutoa zaidi ya shilingi za Kitanzania 900 Billioni katika
mikopo kwa wateja zaidi ya milioni 1.1 wakiwemo wajasiriamali wadogo,
kukuza biashara zao, kutengeneza ajira na kuboresha kiwango cha maisha
yao”.
Katika miaka ijayo FINCA
itaendelea kutekeleza wajibu wake katika kuboresha upatikanaji wa huduma
za kifedha kwa wafanyabiashara wadogo (SMEs) ambao ndio msingi wa
maendeleo ya uchumi wa nchi yetu hasa vijijini.
Ameongeza kuwa FINCA
imejidhatiti katika mpango wake wa kuondoa umasikini kupitia suluhisho
la kudumu ambalo linasaidia watu kujenga rasilimali zao, kutengeneza
ajira na kuboresha kiwango chao cha maisha kiuchumi.
Kwa upande wa Rais na Mkurugenzi
Mtendaji wa FINCA Microfinance Holding Company, Andree Simon aliipongeza
FINCA Tanzania kwa safari yake yenye mafanikio ambayo imewafikisha
katika miaka 20 ya maendeleo na mabadiliko, yaliyosaidia taasisi hiyo
kuendelea kuwa taasisi ya kutoa mikopo midogo na kufikia kuwa Benki ya
kutoa mikopo midogo kama ilivyo sasa.
Mwenyekiti wa Bodi ya FINCA
ambaye pia ni Makamu wa Rais na Mkurugenzi wa Kanda ya Afrika Mike
Gama-Lobo aliwashukuru wajumbe wenzake wa Bodi na viongozi wa juu wa
Benki kwa kuonyesha juhudi za kuigwa ambazo zimepelekea katika kukua kwa
FINCA, kufikia maendeleo makubwa katika mazingira ya biashara yenye
changamoto nyingi.
No comments :
Post a Comment