Waziri wa Mambo ya ndani, Dk
Mwigulu Nchemba amewataka wanafunzi kuachana na harakati za kutengeneza
taswira mbaya za serikali badala yake kuwa na mitazamo chanya.
Aliyasema hayo jana katika
kongamano la UNILIFE lililofanyika Chuo cha Biashara (CBE), ambalo
liliandaliwa na Mbunge wa Viti maalum, Ester Mmasi.
Alisema wanafunzi hawatakiwi
kufanya harakati ili wawe adui wa serikali kwani yenyewe haina muda wa
kushughulikia mashinikizo ya wanafunzi.
“Nilishawahi kufanya harakati
nikiwa chuoni na nilipewa jina la Chifu..majina yangu yamekuja
kujulikana nikiwa serikalini lakini nilikuwa napinga baadhi ya ajenda za
Taifa ambazo niliona hazina manufaa,” alisema Dk Mwigulu.
Alisisitiza kuwa wanafunzi wengi
kwa sasa wamekuwa wakiitafuta taswira mbaya ya serikali bila kuangalia
masuala mengine yanayopaswa kuungwa mkono.
“Kuwa kijana mwema chuoni sio kwa
kuwa kimya Bali kuwa na mitazamo chanya nabukiona mwanazuoni anabisha
jambo jema ujue kuna kasoro,” alisema
No comments :
Post a Comment