Meneja
Uhusiao wa Benki ya CRDB,Godwin Semunyu akizungumza mara baada ya
kuwasilisha mada wakati wa Mkutano Mkuu wa 14 wa Chama cha Maafisa
Habari ,Mawasiliano na Uhusiano Serikalini uliofanyika katika ukumbi wa
Mikutano ya Kimataifa (AICC) jijini Arusha.
Meneja
Uhusiao wa Benki ya CRDB,Godwin Semunyu akiwasilisha mada wakati wa
Mkutano Mkuu wa 14 wa Chama cha Maafisa Habari ,Mawasiliano na Uhusiano
Serikalini uliofanyika katika ukumbi wa Mikutano ya Kimataifa (AICC)
jijini Arusha.
Washiriki
wa Mkutano Mkuu wa 14 wa Chama cha Maafisa Habari ,Mawasiliano na
Uhusiano Serikalini wakifuatilia mada iliyokuwa ikiwasilishwa na Meneja
Uhusiano wa Benki ya CRDB ,Godwin Semunyu wakati wa mkutano huo. kutoka
kulia ni Mwenyekiti wa TAGCO,Pascal Shelutete,Mkurugenzi Mkuu wa Bohari
ya Dawa (MSD) Laurean Bwanakunu na mwisho kushoto ni Katibu Mkuu Wizara
ya Habari ,Sanaa,Utamadunina Michezo,Susan Mlawa.
Baadhi ya Washiriki wa Mkutano huo.
Meneja
Uhusiao wa Benki ya CRDB,Godwin Semunyu akiwasilisha mada juu ya mfumo
maalumu wa kadi za kielektroniki maarufu kama Credit Card ,huduma ambayo
inatolewaa na Benki ya CRDB.
Baadhi
ya Washiriki wa Mkutano mkuu wa 14 wa Chama cha Maafisa Habari
,Mawasiliano na Uhusiano Serikalini (TAGCO) wakifuatilia mada iliyokuwa
ikiwasilishwa na Meneja Uhusiao wa Benki ya CRDB,Godwin Semunyu .
Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii ,Kanda ya Kaskazini .
BENKI
ya CRDB imeahidi kuendelea kukisaidia Chama cha Maafisa Habari
,Mawasiliano na Uhusiano Serikali na kwamba kufanya hivyo kutasaidia
upatikanaji wa taarifa zilizo sahihi na kwa wakati sahihi.
Hayo
yameelezwa na Meneja Uhusiano wa Benki ya CRDB,Godwin Semunyu wakati
akiwasilisha mada wakati wa kikao kazi cha Maafisa Habari ,Mawasiliano
na Uhusiano Serikalini uliofanyika katika ukumbi wa mikutano ya
kimataifa (AICC) jijini Arusha ,sambamba na mkutano mkuu wa chama hicho
(TAGCO)
“Benki
ya CRDB tunaamini “with right information” ambao hawa ni haki yao
kuifikisha kwa wananchi ambao watakuwa aware nini kinaendelea,sio tu
katika kutangaza nafasi za kazi kama baadhi ya watu wanavyofikiria ,pia
wanahusika katika kutangaza Zabuni zilizopo,nafasi za Maendeleo,Nafasi
za uwekezaji na sSehemu gani hasa unaweza kuwekeza kwa ajili ya
maendeleo.”alisema Semunyu.
Amesema
Maafisa Habari wa taasisi za Serikali ndio daraja la kufikisha taarifa
sahihi kwa wananchi na kwamba kupitia kwao kila kinachofanyika ndani ya
Serikali kitwafikia wananchi kwa njia na wakati sahihi.
“Kama
alivyosema Msemaji Mkuu wa Serikali kwamba kuna tofaui kubwa ya
kufikisha habari na kufikisha habari sahihi,kwa hiyo daraja hilo ambalo
kwa muda mrefu limekuwa halipati heshima stahiki sasa litapa
heshima.”alisema Semunyu.
Mwisho







No comments :
Post a Comment