Shirika la Ariel Glaser Pediatric AIDS
Healthcare Initiative (AGPAHI) limekabidhi mashine tano za kuchunguza
saratani ya shingo ya kizazi kwa wanawake ‘cryotherapy machines’ mkoa wa
Mwanza.
Msaada huo umetolewa Jumanne Machi
27,2018 katika ukumbi wa mikutano wa Gold Crest Hotel jijini Mwanza
wakati wa kikao cha wadau wanaohusika katika mapambano ya VVU na Ukimwi
mkoani Mwanza kwa ajili ya kupanga mipango na mikakati ya kupambana na
VVU na Ukimwi.
Akizungumza wakati wa kukabidhi mashine
hizo, Mkurugenzi Mtendaji wa shirika la AGPAHI, Dk. Sekela Mwakyusa
alisema mashine hizo ni kwa ajili ya vituo vya afya vya Katunguru na
Kabila vilivyopo wilaya ya Sengerema, hospitali ya Ngudu iliyopo
wilayani Kwimba na zahanati ya Kirumba na kituo cha afya cha Buzuruga
vilivyopo wilayani Ilemela.
Dk. Sekela alisema mashine hizo tano
zenye thamani ya shilingi milioni 6.8 zitatumika kutolea tiba mgando kwa
akina mama wanaokutwa na dalili za mwanzo za kansa ya uzazi.
“Mbali na shirika letu kuendelea
kuboresha huduma za kinga na matunzo pia tunatoa huduma ya uchunguzi wa
dalili saratani ya mlango wa kizazi kwa akina mama”,alieleza.
Alisema huduma hiyo hutolewa katika vituo vya kutolea huduma ya afya 20 katika mkoa wa Mwanza.
Dk. Sekela alisema shirika hilo mpaka
sasa limetoa msaada wa ‘cryotherapy machines’ 17 katika mikoa sita
ambayo ni Mwanza,Shinyanga,Tanga,Geita,Simiyu na Mara zote zikiwa na
thamani ya jumla ya shilingi milioni 115.6.
Dk. Sekela pia alikabidhi kompyuta 18
zitakazotumika kuhifadhi takwimu za wateja wa CTC katika vituo vya afya
husika na kusaidia upatikanaji wa taarifa kwa haraka na kwa usahihi
Zaidi mkoani Mwanza.
“Tangu tuanze mradi wa Boresha,
tutakuwa tumetoa jumla ya kompyuta 82 kwa mkoa wa Mwanza ambazo
zinatumika kutunza taarifa za watu wenye VVU na Ukimwi”,alisema.
Akizungumza kwa niaba ya wilaya
zilizopokea mashine hizo,Mkuu wa wilaya ya Sengerema Emmanuel Kipole
alilishukuru shirika la AGPAHI kwa kutoa msaada huo na kwamba watatumia
vifaa vilivyotolewa kwa malengo yaliyokusudiwa.
Awali akizungumza katika kikao hicho,
Mkuu wa mkoa wa Mwanza, John Mongella aliwataka wadau wote kuungana na
kushirikiana ili kuhakikisha kuwa maambukizi ya VVU mkoa huo ambayo sasa
ni asilimia 7.2 yanapungua.
AGPAHI ni shirika la Kitanzania
linalofanya kazi kwa kushirikiana na serikali ya Tanzania kutoa huduma
za afya hususani watu wanaoishi na Maambukizi ya Virusi vya Ukimwi na
Ukimwi kwa fadhili wa Watu wa Marekani kupitia Centres for Disease
Control (CDC).
ANGALIA PICHA ZA MATUKIO
Mkuu wa mkoa wa Mwanza, John Mongella
akizungumza katika kikao cha wadau wanaohusika katika mapambano ya VVU
na Ukimwi mkoani Mwanza kabla ya makabidhiano ya kompyuta na mashine
tano za kuchunguza saratani ya shingo ya kizazi kwa wanawake
‘cryotherapy machines’.- Picha zote na Kadama Malunde – Malunde1 blog
Mkurugenzi Mtendaji wa shirika la
AGPAHI, Dk. Sekela Mwakyusa akielezea namna shirika hilo linavyotoa
huduma ya kuwapima saratani ya shingo ya kizazi kwa wanawake.
Dk. Sekela akizungumza na wadau wa afya mkoani Mwanza.
Maboksi yenye kompyuta na mashine za
kuchunguza saratani ya shingo ya kizazi kwa wanawake ‘cryotherapy
machines’ zilizotolewa na shirika la AGPAHI kwa ajili ya vituo vya afya
mkoani Mwanza.
Kulia ni Dk. Mwakyusa akiwa ameshikilia
moja ya mashine inayotumika kuchunguza saratani ya shingo ya kizazi kwa
wanawake ‘cryotherapy machines’.
Dk. Sekela akizungumza ukumbini.
Katikati ni Dk. Sekela Mwakyusa
akikabidhi mashine kwa Mkuu wa mkoa wa Mwanza,John Mongella (wa pili
kushoto) na viongozi wa wilaya ya Sengerema.
Zoezi la makabidhiano likiendelea. Wa kwanza kushoto ni Mwakilishi wa CDC nchini, Dk. Eva Matiko.
Kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Nyamagana, Mary Tesha akipokea cryotherapy machine.
Mkuu wa wilaya ya Sengerema Emmanuel
Kipole akitoa neno la shukrani baada ya makabidhiano ya mashine tano za
kuchunguza saratani ya shingo ya kizazi kwa wanawake na kompyuta 18
zilizotolewa na shirika la AGPAHI.
Picha zote na Kadama Malunde – Malunde1 blog
No comments :
Post a Comment