Friday, February 2, 2018

WAZIRI MPINA AKAMATA MELI YA UVUVI HARAMU NA KUITOZA FAINI YA MILIONI MIA SABA SABINI

 Waziri wa Mifugo
na Uvuvi Luhaga Mpina akiangalia  mzigo wa mapezi  ya samaki
aina ya papa wakati Kapteni Han Ming Chuan wa Meli ya Buah Naga 1 akifungua
mfuko wenye Mapezi yaliyokamatwa kinyume na  Sheria yaUsimamizi
wa Bahari Kuu(DSFA) ya Mwaka 1998  kama ilivyorekebishwa Mwaka
2007.Meli hiyo ilitozwa faini ya shilingi milioni 770. Picha na John
Mapepele
 Waziri wa Mifugo
na Uvuvi Luhaga Mpina akiangalia pezi  la samaki aina ya papa wakati
alipokagua Meli ya Buah Naga 1 yenye Mapezi yaliyokamatwa kinyume na
Sheria yaUsimamizi  wa Bahari Kuu(DSFA) ya Mwaka 1998  kama
ilivyorekebishwa Mwaka 2007.Meli hiyo ilitozwa faini ya shilingi milioni
770. Picha na John Mapepele
 Waziri wa Mifugo
na Uvuvi Luhaga Mpina akitoka kwenye Meli ya Buah Naga 1 baada ya kuikagua
ambapo ilikutwa na mapezi ya samaki aina ya papa kinyume na  Sheria
yaUsimamizi  wa Bahari Kuu(DSFA) ya Mwaka 1998  kama ilivyorekebishwa
Mwaka 2007.Meli hiyo ilitozwa faini ya shilingi milioni 770. Picha na
John Mapepele
Meli ya Buah
Naga 1 iliyokamatwa eneo la Mtwara ikiwa na kilo 90 ya mapezi ya samaki
aina ya papa yaliyokamatwa kinyume na  Sheria yaUsimamizi
wa Bahari Kuu(DSFA) ya Mwaka 1998  kama ilivyorekebishwa Mwaka
2007.Meli hiyo ilitozwa faini ya shilingi milioni 770. Picha na John
Mapepele
Na
John Mapepele, Mtwara


Waziri wa Mifugo
na Uvuvi Luhaga Mpina ameridhia utozwaji wa faini ya dola za kimarekani
laki tatu na nusu sawa na shilingi milioni mia saba  na sabini
iliyotozwa na Mamlaka ya Usimamizi wa Bahari Kuu (DSFA)  kwa Meli
ya Buah Naga 1 kutoka nchini Malaysia  kwa kosa la kukutwa
mapezi ya  samaki aina ya papa kilo 90 huku miili ya samaki hao
kutupwa baharini kinyume na kanuni ya 66 ya kanuni za bahari kuu za
mwaka 2009 na kifungu namba 18(2) cha  Sheria yaUsimamizi
wa Bahari Kuu(DSFA) ya Mwaka 1998 kama ilivyorekebishwa Mwaka
2007.
Akizungumza
baada
ya kukagua meli hiyo leo mjini Mtwara, Waziri Mpina alisema kuwa
wamiliki  wa meli hiyo wanatakiwa kulipa faini hiyo ndani ya siku
saba ambapo kama hawatalipwa watapelekwa mahakamani mara moja na kushtakiwa
kwa mujibu wa sheria za nchi.
Aidha Mpina amesema
Serikali imetaifisha tani nne na nusu za samaki ambazo zitauzwa mara
moja kwa njia ya mnada na kwa kuzingatia taratibu mbalimbali za
Serikali.
Akitoa taarifa ya
kukamatwa
kwa meli hiyo, kwa Waziri, Kiongozi wa Kikosi Kazi maalum cha kudhibiti
uvuvi haramu, Kamishna  Frederick Milanzi wa Tume ya Kupambana
na Madawa ya Kulevya nchini amesema kwamba Kapteni wa meli hiyo Han
Ming Chuan raia wa Malaysia  alikutwa  na bastola  aina
ya Bereta na risasi kumi ambayo alikuwa anaimiliki kinyume cha
sheria.
Amesema kuvua na
kutupa
mizoga ya samaki baharini siyo tu kwamba wanahujumu  raslimali
za uvuvi baharini bali pia wanachangia  katika uchafuzi wa mazingira
ya baharini.
Pia Waziri Mpina
amesisitiza
kuwa Serikali haipo tayari kufanya kazi  na wawekezaji wababaishaji
kwenye sekta ya uvuvi na kwamba kuanzia sasa  hatua kali za kisheria
zitachukuliwa kwa  yeyote atakayejaribu kuhujumu raslimali za uvuvi
na kujihusisha na uvuvi haramu.
Aidha Waziri
Mpina
ametoa onyo kali kwa wawekezaji wa uvuvi kwenye bahari ya Tanzania kuacha
kutumia mwanya wa kupewa kibali cha kuvua na kujihusisha na  makosa
mbalimbali.
Ameyataja  baadhi
ya makosa  hayo kuwa ni pamoja na usafirishaji haramu wa silaha,
binadamu, madawa ya kulevya na nyara za serikali ikiwemo meno ya tembo.
Pia usafirishaji wa  mazao ya misitu na
samaki.
Kwa upande wake, Bw.
Wankyo Simon ambaye ni Wakili wa Serikali kutoka Ofisi ya Mwanasheria
Mkuu wa Serikali Divisheni ya Mashtaka Makao Makuu Dar es Salaam na
Mkuu wa Dawati linalohusiana na Makosa ya Mazingira, amesema makosa
ya namna hii ni makubwa na endapo kiwango hicho cha pesa hakitalipwa
kama ilivyoamriwa, taratibu za kiupelelezi zitakamilishwa na kapteni
wa Meli hiyo atafikishwa mahakamani kwa makosa yaliyoainishwa ambapo
anaweza kupewa adhabu ya kifungo na meli hiyo kutaifishwa na kuwa mali
ya Serikali. 
Pia amependekeza
kuwepo
kwa mwongozo wa uendeshaji mashauri (Standard Operating Procedures)
kwa makosa yanayofanyika baharini ili uweze kutumiwa na wadau mbali
mbali kuanzia ukamataji wa chombo husika, upelelezi wake, namna bora
ya kutunza chombo hicho na uendeshaji wa mashauri yanayotokana na operesheni
zote zinazofanyika baharini. 
Alisema mwongozo
utasaidia
kuimarisha kesi zote zinazoenda mahakamani kuanzia inapofunguliwa mpaka
kufikishwa mahakamani na wadau wote watajua kwa urahisi namna ya kusimamia
utekelezaji wa majukumu yao.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu
wa (DSFA) Hosea Mbilinyi amesema Mamlaka yake imegundua kuwepo kwa
baadhi ya wawekezaji wasiofuata taratibu na Sheria  za kufanya
shughuli za uvuvi katika bahari ya Tanzana  ambapo amesema tayari
Mamlaka imeshawapiga faini ya dola za kimarekani laki moja kwa meli
tatu zilizofanya makosa katika sikuza hivi
karibuni.
Katika siku za hivi
karibuni Waziri wa Mifugo na Uvuvi ameunda  timu iliyoshirikisha
wataalam kutoka katika vyombo mbali vya Serikali kuendesha operesheni
maalum ya kutokomeza uvuvi haramu nchini ambayo  licha ya kupata
mafanikio makubwa imetoa hamasa kwa wavuvi  kuanza kusalimisha
zana haramu za uvuvi  na kuziteketeza.

No comments :

Post a Comment