Madaktari Bingwa wa Magonjwa ya Moyo kutoka Taasisi ya Moyo Jakaya
Kikwtete (JKCI) Peter Kisenge na Prof. Ahmed Osman wa Broward General
Medical Centre ya nchini Marekani wakimfanyia mgonjwa upasuaji wa Moyo
wa bila kufungua kifua na kumuwekea kifaa maalum cha kuusaidia moyo
kufanya kazi vizuri (pace maker) ikiwa ni sehemu ya mafunzo kwa vitendo yaliyoandaliwa na kampuni ya Medtronic tawi la Kenya ambao ni watengenezaji wa vifaa tiba vya magonjwa ya Moyo.
Prof.
Ahmed Osman kutoka Broward General Medical Centre ya nchini Marekani
akizungumza na viongozi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wakati
wa mafunzo ya mfumo wa umeme wa Moyo (Electrocardiogram –ECG) kwa wafanyakazi wa Taasisi hiyo yaliyoandaliwa na kampuni ya Medtronic tawi la Kenya ambao ni watengenezaji wa vifaa tiba vya magonjwa ya Moyo.
Viongozi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa kampuni ya Medtronic ambao ni watengenezaji wa vifaa tiba vya magonjwa ya Moyo wakati wa mafunzo ya mfumo wa umeme wa Moyo (Electrocardiogram – ECG) kwa wafanyakazi wa JKCI yaliyoandaliwa na kampuni hiyo.
Prof. Ahmed Osman kutoka Broward General Medical Centre ya nchini Marekani akiwafundisha wafanyakazi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) jinsi mfumo wa umeme wa Moyo (Electrocardiogram –ECG) unavyofanya kazi mwilini wakati wa mafunzo hayo yanayoenda sambamba na vitendo ya siku tano yaliyoandaliwa na kampuni ya Medtronic tawi la Kenya ambao ni watengenezaji wa vifaa tiba vya magonjwa ya Moyo.
Wafanyakazi wa Taasisi ya Moyo
Jakaya Kikwete (JKCI) wakimsikiliza Prof. Ahmed Osman (hayupo pichani)
kutoka Broward General Medical Centre ya nchini Marekani akiwafundisha
jinsi mfumo wa umeme wa Moyo (Electrocardiogram -ECG) unavyofanya kazi
mwilini.
Picha na JKCI
No comments :
Post a Comment