Mheshimiwa Matilda Masuka Balozi
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Jamhuri ya Korea
akiwakaribisha na kuwashukuru wageni waalikwa waliohudhuria kwa wingi
kwenye ufunguzi rasmi wa Ofisi za Ubalozi tarehe 31 Januari 2018. Awali
Tanzania ilikuwa inawakilishwa nchini humo kutokea Japan. Mheshimiwa
Balozi Matilda Masuka aliteuliwa Desemba 3, 2016 na baadaye kuapishwa
kuwa Balozi wa kwanza mwenye makazi yake Mji Mkuu wa Seoul, Jamhuri ya
Korea.
Mheshimiwa Lim Sung-nam, Naibu
Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Korea akizungumza kwa niaba ya
Serikali yake wakati wa ufunguzi rasmi wa Ubalozi wa Tanzania nchini
humo. Kwenye salamu zake za ufunguzi, Mheshimiwa Sung-nam amesifu
jitihada za Serikali ya Tanzania kukuza uchumi na kusifu ushawishi na
karisma ya Balozi Masuka ambayo imewezesha kuvutia Mabalozi na
wanadiplomasia wengi Jijini Seoul kushuhudia ufunguzi wa ofisi za
Ubalozi.
Mheshimiwa Ban Ki-moon, Katibu
Mkuu wa Umoja wa Mataifa Mstaafu akihutubia wageni waliofika kwenye
Ofisi za Ubalozi wa Tanzania. Mheshimiwa Ki-moon, ambaye alitambulishwa
kama rafiki mkuu wa Tanzania nchini humo, alipongeza Serikali ya
Tanzania kwa kufanikiwa kusimika bendera ya Tanzania nchini mwake baada
ya miaka 25 ya uhusiano mzuri wa kidiplomasia na ushirikiano wa
kiuchumi.
Picha ya pamoja baada ya Waziri
Mahiga na Mheshimiwa Sung-nam kukata utepe na kuzindua rasmi majengo
hayo. Kutoka kushoto ni Bw. Park Young min, Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya
Afrika; Mhe. Silvester Bile, Kiongozi wa Mabalozi wa Afrika na Balozi wa
Ivory Coast; Mhe. Ban Ki-moon, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Mstaafu;
Mhe. Augustine Mahiga, Waziri wa Mambo ya Nje Tanzania; Mhe. Lim
Sung-nam, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje Korea Kusini; Mhe. Matilda
Masuka, Balozi wa Tanzania nchini Korea Kusini; na Mhe. Salim Alharthy,
Kiongozi wa Mabalozi na Balozi wa Falme ya Oman nchini Korea ya Kusini.
Picha ya pamoja na Mabalozi
wanawake wanaoziwakilisha nchi mbalimbali kwenye Jamhuri ya Korea na
picha ya Mabalozi kutoka nchi za kiafrika walioko nchini Korea Kusini.
No comments :
Post a Comment