Tuesday, February 27, 2018

TTCL CORPORATION YAJA NA HUDUMA MPYA YA (Fiber Connect Bundle), INA KASI YA AJABU


kin1
Waziri Waziri Kindamba Mkurugenzi MKuu wa Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL CORPORATION) akizungumza na waandishi wa habari katika makao makuu ya shirika hilo Jengo la Extelecoms Mtaa wa Samora jijini Dar es salaam kulia ni Bw.Ali Mbega Mkuu wa Mauzo na Masoko (TTCL CORPORATION)
kin2
Waziri Waziri Kindamba Mkurugenzi MKuu wa Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL CORPORATION)akimzikiliza Ali Mbega Mkuu wa Mauzo na Masoko (TTCL CORPORATION) wakati alipokuwa akijibu moja ya swali yaliyoulizwa na waandishi wa habari katika mkutano huo.
kin3
Waziri Waziri Kindamba Mkurugenzi MKuu wa Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL CORPORATION)akijibu maswali katika mkutano huo pamoja na  Ali Mbega Mkuu wa Mauzo na Masoko (TTCL CORPORATION) na maafisa wengine wa shirika hilo.
……………………………………………………………………………..
Waziri Waziri Kindamba  Mkurugenzi Mkuu wa (TTCL CORPORATION)  leo amezindua  huduma  mpya  ya kampuni hilyo iliyopewa jina la Fiber Connect Bundle, Amesema huu ni mwendelezo wa ubunifu wa Kampuni yenu ya kizalendo katika kuwapatia huduma za kipekee kabisa.
Kindamba amesema TTCL Corporation imechukua hatua ya kuwafuata nyumbani na kufanya mapinduzi makubwa ya kimawasiliano. Kupitia huduma hii mpya ya Fiber Connect Bundle, ambapo mteja  atapata huduma nne kwa pamoja zikiwa na unafuu mkubwa wa gharama na ubora wa hali ya juu.
Amesema kwa kuanzia, mradi unatarajiwa kufikisha huduma katika nyumba zipatazo 500 katika eneo la Mikocheni,   Nyumba 500 zingine katika eneo la Mbezi Beach na nyumba zaidi ya 200 katika eneo la Medeli Mkoani DODOMA.
Ameongeza kwamba Kupitia kifurushi cha Fiber Connect, Mteja ataweza kufaidika na huduma zifuatazo; Kwanza, Mteja atapata Intaneti yenye kasi isiyo na kikomo( Unlimited). Pili, Mteja atapata huduma ya simu za sauti kwa simu za mezani na (Sim Card) ambayo ataitumia kwenye simu yake ya mkononi na kupata huduma ya Intaneti sawa na simu ile anayopata katika simu ya mezani.
Akizungumzia  mwelekeo wa utendaji wa Shirika  amesema unaonesha ukuaji mzuri licha ya changamoto zilizopo. Mapato yameendelea kuongezeka na hasara kupungua kwa kiasi kikubwa, jambo linalotupa uhakika wa kutimiza ahadi yetu ya kutoa gawio Serikalini katika mwaka huu wa fedha 2017/2018.
“Mtakumbuka kuwa, kwa zaidi ya miaka kumi na tano iliyopita, TTCL haikuawahi kutoa gawio. Tumedhamiria kuvunja mwiko huu kwa kutimiza ahadi yetu kwa Umma ya kutoa gawio la shilingi Bilioni moja katika mwaka huu wa fedha” Aemesema Kindamba.
Menejimenti itaendelea kuweka mkazo katika kuboresha eneo la Huduma kwa Wateja kwa kutoa huduma bora kwa gharama nafuu, kuongeza Wateja wapya, kusambaza huduma za 4G LTE katika Makao Makuu ya Mikoa yote Nchini ifikapo Juni 2018.
Aidha, tutaendelea kuongeza uwekezaji katika Teknolojia na Miundo mbinu yetu kote nchini, kuboresha mazingira ya kazi kwa Wafanyakazi na Vitendea kazi, kukusanya Madeni ya Shirika, kuongeza Wateja na ufanisi katika huduma za fedha Mtandao (TTCL PESA) na kuongeza ufanisi katika Miundombinu ya Kimkakati ya Serikali inayosimamiwa na kuendeshwa na Shirika la Mawasiliano Tanzania na hapa ninazungumzia Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano (NICTBB) na Kituo Mahiri cha kuhifadhia Kumbukumbu(National Data Centre).
Huduma ya tatu , Mteja atapata huduma za wireless service (WiFi) katika nyumba yake ambapo vifaa vyote vinavyotumia Teknolojia ya Intaneti vitaunganishwa na kuweza kutumia huduma hii. Mfano wa vifaa husika ni Smart Tv, Tablets, Laptops na kadhalika
Nne, Mteja atapatiwa vifaa  vyote bure pamoja na uhakika wa huduma za baada (After Sells Services) endapo itahitajika
Mchanganuo wa gharama na mgawanyiko wa kifurushi hiki ni kama ifuatavyo
Jina la Kifurushi                   Muunganiko wa Huduma   Gharama   Matumizi
Kasi ya Intaneti (Mbps) Dakika za maongezi Mitandao yote
Fiber Connect Lite 10 50 100,000.00   Siku 30
Fiber Connect Basic 30 100 150,000.00
Fiber Connect Preffered 50 300 200,000.00
Ili kupata huduma ya kifurushi hiki maalumu cha FTTH, Mteja unapaswa kufanya yafuatayo; Piga namba 100/ 022214100100 kuongea na Wahudumu wetu au
Tembelea kituo  chetu cha Huduma kwa Wateja kilicho karibu nawe.
Huduma hii inazilenga:  Taasisi zote za Serikali, Wafanyabiashara wakubwa, wa kati na wadogo na Ofisi mbalimbali.

No comments :

Post a Comment