Mwenyekiti wa Halmashauri ya
wilaya ya Misungwi, Anthony Bahebe akiwa chini ya ulinzi baada ya
kukamatwa na Jeshi la Poli kwa kushirikiana na Taasisi ya Kuzuia na
Kuapamba na Rushwa Tanzanai (TAKUKURU) jijini Mwanza Februari 21, 2018
kwa tuhuma za matumizi kabaya ya madaraka na ubadhilifu wa fedha za
umma.
Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu
…………….
JESHI la Polisi mkoani Mwanza kwa
kushirikiana na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Tanzania
(TAKUKURU) mkoani hapa imemkamata Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya
ya Misungwi Bw. Anthony Bahebe.
Pia Mwanasheria wa Halmashauri hiyo Bw.
Alphonce Sebukoto naye amekamatwa na Jeshi hilo. Viongozi wote hao
wanakabiliwa na tuhuma za matumizi mabaya ya madaraka na ubadhilifu wa
fedha za umma.
Akizungumza na waandishi wa habari,
Kamanda wa Polisi wa mkoa wa Mwanza, Ahmed Msangi alisema kukamatwa kwa
viongozi hao kunatokana na tuhuma mbalimbali zinazowakabili ikiwa ni
pamoja na matumizi mabaya ya madaraka.
Kamanda Msangi alisema, Bw. Sebukoto
alikamatwa Februari 19, 2017 na Bw. Bahebe amekamatwa leo na wote
wanaendelea kuhojiwa na Polisi kwa kushirikiana na TAKUKURU.
Naye Kamanda wa TAKUKURU wa mkoa
wa Mwanza Mhandisi Ernest Makale alisema Bw. Sebukoto aliidhinisha
malipo ya sh.milioni 278 zilipwe katika akaunti binafsi ya Mwenyekiti wa
Halmashauri hiyo Bw. Bahebe.
Alisema Bw. Sebukoto aliidhinisha
malipo hayo kwa Bw. Bahebe Novemba 2017 wakati alipokuwa anakaimu nafasi
ya ukurugenzi wa Halmashauri ya Misungwi ambapo jumla sh. milioni 138
ziliingizwa katika akaunti binafsi ya Mwenyekiti huyo. Alisema kiasi
kingine cha fedha kinachunguzwa kubaini kilipo.
Kukamatwa kwa viongozi hao kunatokana na
juhudi za Serikali katika mapambado dhidi ya matumizi mabaya ya madaraka
pamoja na fedha za umma.
Februari 19, 2019 akiwa katika ziara yake
wilayani Misungwi Waziri Mkuu Kassim Majaliwa alimsimamisha kazi
Mwanasheria wa Halmashauri ya wilaya ya Misungwi Bw. Sebukoto na kuagiza
achungunzwe na vyombo husika.
Alichukua hatua hiyo baada
Mwanasheria huyo kushindwa kutekeleza majukumu yake ipasavyo ikiwa ni
pamoja na kushindwa kuishauri vyema halmashauri hiyo na kuisababishia
hasara ya sh. milioni 278.
Amesema Mwanasheria huyo Novemba
2017 wakati alipokuwa anakaimu nafasi ya ukurugenzi aliidhinisha malipo
ya sh.milioni 278 zilipwe katika akaunti binafsi ya Mwenyekiti wa
Halmashauri hiyo Bw. Anthony Bahebe.
Waziri Mkuu alisema Bw. Bahebe
aliishtaki halmashauri hiyo akidai kulipwa fedha kwa ajili ya kazi ya
ukandarasi wa mradi wa maji Igenge uliojengwa na kampuni ya ukandarasi
ya Seekevim.
Alisema mradi huo ulianza 2014 na
ulitakiwa ukamilike 2015. Mwanasheria huyo aliidhinisha malipo hayo
wakati ambao tayari hati maalumu ya uwakilishi ilikuwa imekwisha tangu
Desemba 2015.
Alisema Mwanasheria alimlipa
Mwenyekiti wa Halmashauri kwa kufanya kazi na Halmashauri jambo ambalo
ni kinyume na maadili ya utumishi wa umma.
Hivyo alitumia fursa hiyo
kuwakumbusha watumishi wa umma kuzingatia maadili ya utumishi na matakwa
ya kisheria katika utekelezaji wa majukumu yao.
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
JUMATANO, FEBRUARI 21, 2018.
No comments :
Post a Comment