Wednesday, February 21, 2018

Mkutano wa Majadiliano ya Miundombinu,Fedha na Afya wafanyika Uganda


1
Waziri wa Nishati Mhe. Medadi Kalemani akizungumza na Katibu Mkuu wa Wizara ya Wizara  ya Nishati Dkt. Hamisi Mwinyinvua kabla ya kuanza kwa Mkutano wa Majadiliano wa Miundombinu ya Uchukuzi, Fedha  na Afya leo unaofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Speke Resort  Munyonyo- Uganda ambao utafuatiwa na Mkutano Kazi kesho wa Wakuu wa Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki. Kushoto ya Mhe. Waziri wa Nishati ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Adolf Mkenda.
2
Kushoto katika picha ni Mhandisi Joseph Nyamhanga Katibu Mkuu  Ujenzi, pembeni yake Prof. Joseph Buchweishaija Naibu Katibu Mkuu Prof. Joseph Buchweishaija, Bi.  Amina Kh. Shabaan Naibu Katibu Mkuu, Fedha na Mipango na kulia katika picha ni Mhandisi Shomar O. Shomari Naibu Katibu Mkuu, Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi Zanzibar ni washiriki katika wa Mkutano wa Majadiliano wa Miundombinu ya Uchukuzi, Fedha  na Afya  unaoendelea kufanyika katika ukumbi wa mikutano wa Speke Resort  Munyonyo-Uganda
                                            
                                         Picha na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki

No comments :

Post a Comment