Tuesday, February 27, 2018

ISAKA KUJENGWA KIWANDA CHA KUSANIFU MABOMBA YA MAFUTA


PICHA MOJA
Waziri wa Nishati ,Dkt. Medard Kalemani (kulia)akiteta jambo na mkuu wa mkoa wa shinyanga Zainabu Tellack wakati wa warsa ya wadau wa bomba la kusafirisha mafuta ghafi kutoka Hoima Uganda hadi bandari ya Tanga nchini Tanzania uliofanyika wilayani Kahama mkoani Shinyanga
PICHA MBILI
Waziri wa Nishati ,Dkt. Medard Kalemani (wa tatu kulia waliokaa) na Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Wiliam Lukuvi wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi mbalimbali wa Wilaya ya Kaham mkoa wa shinyanga wakati wa warsa ya wadau wa bomba la kusafirisha mafuta ghafi kutoka Hoima Uganda hadi bandari ya Tanga Tanzania uliofanyika mkoani
PICHA TATU
Waziri wa Nishati ,Dkt. Medard Kalemani( wa pili),waziri wa ardhi, nyumba na maendeleo ya makazi Wiliam Lukuvi na Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Zainabu Tellack wakati warsa ya wadau wa bomba la kusafirisha mafuta ghafi kutoka Hoima Uganda hadi bandari ya Tanga Tanzania uliofanyika mkoani Shinyanga.
PICHAA NNEE
Katibu Mkuu wa wizara ya Nishati, Dkt. Hamis Mwinyimvua (kushoto) na Kaimu Kamishna wa Nishati na Maendeleo ya Petroli Mhandisi Innocent Luoga( kushoto) wakizungumza na Katibu Tawala wa Mkoa wa Shinyanga Albert Msovela( katikati) nje ya ukumbi wakati warsa ya wadau wa bomba la kusafirisha mafuta ghafi kutoka Hoima Uganda hadi bandari ya Tanga Tanzania uliofanyika mkoani Shinyanga
……………….
Wakazi wa Shinyanga watakiwa changamkia fursa za ajira
Na Zuena Msuya Kahama, Shinyanga,
Waziri wa Nishati ,Dkt. Medard Kalemani amesema kiwanda kikubwa cha kusanifu mabomba yatakayotumika katika ujenzi wa bomba la kusafirisha mafuta ghafi kutoka
Hoima nchini uganda hadi katika bandari ya Tanga nchini Tanzania kitajengwa katika mji wa Isaka wilayani Kahama mkoani  Shinyanga .
Vile vile alieleza kuwa Wilaya ya Kahama ni miongoni mwa Wilaya 24 nchini zitakazopitiwa na Mradi wa Ujenzi wa Bomba hilo la kusafirisha mafuta ghafi kutoka nchini Uganda hadi Tanzania .
Kufuatia ujenzi wa kiwanda hicho pamoja na utekelezaji wa mradi wa bomba, Dkt Kalemani aliwataka wakazi wa Mkoa wa Shinyanga kuchangamkia fursa za ajira kwa kuwa zitatoa kipaumbele kwa watanzania.
Dkt. Kalemani alisema hayo wakati wa Warsha ya Wadau wa Bomba la Kusafirisha  Mafuta ghafi Afrika Mashariki iliyofanyika wilayani Kahama mkoani Shinyanga,kwa lengo la kutoa elimu na kueleza hatua iliyofikiwa katika maendeleo ya utekelezaji wa mradi.
Akizungumzia suala la ajira, Dkt. Kalemani alifafanua kuwa zaidi fursa ya ajira na ajira elfu kumi( 10,000) zitapatikana wakati wa utekelezaji wa mradi wa  ujenzi wa bomba hilo ambazo zitatoa kipaumbele kwa watanzania wenye sifa na taaluma husika pia kwa wale wasio na taaluma kwa kuwa kuna kazi nyingine zisizohitaji taaluma.
” Wakazi wa Kahama changamkieni fursa za ajira na shughuli mbalimbali za kuwaingizia kipato, sitarajii kuona watanzania wakikosa ajira,kazi zitakuwa nyingi sana kwa wenye sifa na wasio na sifa, tijitume na tuwe wabunifu zaidi mradi huu ni kwa manufaa yetu sisi,” alisisitiza Dkt. Kalemani
Aidha alisema kuwa kuwepo kwa mradi huo kuitaingizia Serikali mapato yatokanayo shughuli mbalimbali za kibiashara zitakazo kuwa zikifanyika katika eneo hilo.
Kuhusu hatua iliyofikiwa katika maendeleo ya utekelezaji wa mradi huo, Dkt. Kalemani alisema kuwa ujenzi rasmi wa Mradi wa Bomba la kusafirisha mafuta ghafi unatarajiwa utaanza mwezi Mei mwaka huu na kwa sasa kinachoanyika ni  kuchukuwa sampuli ya tathmini ya namna ya ulipaji wa fidia kwa wananchi watakaopitia na mradi huo.
“tone la kwanza la mafuta litadondoka 2020, huu ni uwekezaji mkubwa sana, tuipondeze serikali ya awamu ya tano kwa kuhakikisha mradi huu unakuja Tanzania, nchi nyingi ziliuhitaji, wananchi tuunze na kuulinda mradi wetu”, alisisitiza Dkt. Kalemani.
Bomba hilo lenye urefu wa kilometa 1443 litajengwa kwa kipindi cha miaka mitatu (3) na linatarajiwa kukamilika ifikapo mwaka 2020 litakuwa na uwezo wa kusafirisha mapipa 216,000 kwa siku.
Katika hatua Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu aliwataka wanawake kuchangamkia fursa ya ajira na biashara katika mradi huo wa bomba kwa kuwa wanawake wengi wamekuwakibaki nyuma.
hivyo amewaasa viongozi hasa wale wanawake kutoa hamasa kwa wanawake wote ambapo maeneo yatapitiwa na bomba la mafuta kufanya kila jitihada ili waweze kunufaika kiuchumi kupitia mradi huo kwa kufanya shughili mbalimbali ikiwemo biashara ndogo.

No comments :

Post a Comment