Mheshimiwa Dkt. Augustine Mahiga,
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki akipokelewa na
maua na Mheshimiwa Matilda Masuka, Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania kwenye Jamhuri ya Korea Kusini. Kushoto ni Ndugu Masuka, mume
wa Balozi Masuka.
Mheshimiwa Dkt. Augustine Mahiga,
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki akisalimiana
na wawakilishi wa kampuni ya GS E&C waliofika hotelini kwake na
kufanya naye mazungumzo ya kikazi kwenye Mji Mkuu wa Jamhuri ya Korea,
Seoul. Pichani wawili ni Mkurugenzi Mkuu wa Makampuni hayo Bw. Min
Jeoung.
Picha ya pamoja.
Ujumbe wa Mheshimiwa Mahiga
ukiongozwa na Mheshimiwa Matilda Masuka, Balozi wa Tanzania nchini Korea
Kusini, Bw. Geoffrey Mwambe, Mkurugenzi Mtendaji wa TIC na Bw. Edwin
Rutageruka, Mkurugenzi Mkuu wa TANTRADE wakiwa kwenye mazungumzo na
wawakilishi wa makampuni ya GS E&C.
……………………
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Dkt. Augustine Mahiga ameanza ziara ya kikazi ya siku tatu nchini Jamhuri ya Korea Kusini yenye lengo la kuimarisha uhusiano wa kidiplomasia na kiuchumi baina ya Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania na Jamhuri ya Korea ya Kusini.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Dkt. Augustine Mahiga ameanza ziara ya kikazi ya siku tatu nchini Jamhuri ya Korea Kusini yenye lengo la kuimarisha uhusiano wa kidiplomasia na kiuchumi baina ya Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania na Jamhuri ya Korea ya Kusini.
Mara baada ya kuwasili kwenye
Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Incheon Mjini Seoul, Mheshimiwa Waziri
Mahiga amekutana na kufanya mazungumzo na Mkurugenzi Mkuu wa Makampuni
ya GS E&C Bw. Min Jeong na timu yake inayoshugulikia uwekezaji na
biashara nchini Tanzania.
Waziri Mahiga aliyeongozana na
Bw. Edwin Rutageruka, Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Maendeleo ya
Biashara (TANTRADE) na Bw. Geoffrey Mwambe, Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo
cha Uwekezaji cha Tanzania alielezea utayari wa Tanzania kutekeleza
miradi mikubwa ya maendeleo kama ule wa ujenzi wa reli ya kisasa ya
viwango vya kimataifa wa “Standard Gauge Railway” inayohusisha makampuni makubwa ya kimataifa.
Kwa upande wake Mkurugenzi
Jeong alielezea kuwa Kampuni ya GS E&C iliyojikita kwenye ujenzi wa
miundombinu ya viwango vya kimataifa, ufuaji na usambazaji wa umeme,
usafishaji wa mafuta n.k., sasa imejipanga pia kushiriki katika Ujenzi
wa SGR (kupitia ushirikiano na kampuni ya Uturuki (awamu ya 3-5), na
Ujenzi wa Daraja la Selanda.
Mbali na mpango huo, kwa sasa
Kampuni hiyo yenye makao yake makuu kwenye mji mkuu wa Korea Kusini,
Seoul, imeshiriki katika Mradi ya Umeme nchini Tanzania wa Dar-Arusha
“Transmition Line”.
Waziri Mahiga alisisitiza nia
ya dhati ya Serikali ya Tanzania katika kusimamia ujenzi wa Reli ya
Kisasa ya Viwango na kuhakikisha inakamilika kwa wakati. Vilevile
alitumia fursa hiyo kumuelezea Mkurugenzi Jeong na timu yake kuhusu
mpango wa uendelezaji wa ujenzi wa reli hiyo ya viwango kutoka Isaka
hadi Kigali, mpango ambao ulitangazwa na Waheshimiwa John Pombe Joseph
Magufuli na Mheshimiwa Paul Kagame, Rais wa Tanzania na Rwanda hivi
karibuni.
Mheshimiwa Mahiga alimhakikishia
mkurugenzi huyo na kundi la makampuni anayoyaongoza, ushirikiano wake na
kumkaribisha kuwekeza zaidi nchini Tanzania kwenye miradi mbalimbali ya
umeme na miundombinu mingine.
Kampuni ya GS E&C ni miongoni mwa makampuni kumi “Top Ten” yanayofanya vizuri zaidi nchini Korea Kusini inayokusanya faida ya kiasi cha $10 bilioni kwa mwaka.
Mheshimiwa Waziri Mahiga
ambaye yupo nchini hapa kuanzia leo tarehe 30 Januari hadi tarehe 2
Februari, 2018, kufuatia mwaliko wa Mhe. Dkt. Kang Kyung-wha, Waziri wa
Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Korea anatarajiwa pia kuzindua Kongamano la
kwanza la wafanyabiashara, kufungua majengo ya Ubalozi wa Tanzania na
kufanya mazungumzo maalum na mwenyeji wake Waziri Kang Kyung-wha.
Mheshimiwa Mahiga atatumia
sehemu kubwa ya ziara hiyo kukutana na kufanya mazungumzo na makampuni
makubwa yalikwisha onesha nia ya kuwekeza nchini Tanzania. Mwishoni mwa
ziara hiyo, Mheshimiwa Waziri Mahiga anategemewa kutembelea Chuo cha
Taifa cha Diploamasia cha Korea Kusini, kabla ya kurejea nchini
Tanzania.
-Mwisho-
Imetolewa na:Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali,
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,
Seoul, Korea Kusini,
30 Januari 2018.
No comments :
Post a Comment