Waziri Afya, Maendeleo ya
Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Ummy Mwalimu akikagua huduma za afya kwenye
kituo cha afya cha kamanga kilichopo Wilaya ya Sengerema.Waziri ummy
yupo Mkoani Mwanza katika ziara ya kikazi ya kujionea hali ya utoaji
huduma za afya mkoani hapo.
Waziri ummy Mwalimu akiangalia
ramani ya kituo hicho cha afya ambacho kimejengwa kwa ushirikiano wa
Halmashauri ya Wilaya ya Sengerema na Shirika la SEDA Foundation, kulia
ni Mganga Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Dkt.Subi na kushoto ni mmoja wa
Viongozi wa Shirika hilo.
Waziri Ummy Mwalimu akiangalia
Ramani ya Ujenzi wa jengo la ghorofa nne la Uzazi linalojengwa hospitali
ya Mkoa ya Sekoture jijini Mwanza.
Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na watoto akiangalia kazi inavyoendelea katika hospitali hiyo
Waziri Ummy Mwalimu akiangalia
duka la dawa lililopo kwenye hospitali ya Mkoa ya Sekoture ambapo
upatikanani wa dawa kwa Mkoa wa Mwanza ni asilimia 80.
Mawaziri hao wakijadili jambo
wakati wa ukaguzi wa jengo la upasuaji wa kumtoa mtoto tumboni
linalojengwa kwenye kituo cha afya cha Karume ,Wilayani Ilemela
…………….
Na.WAMJW,Mwanza
Wakurugenzi wa Halmashauri nchini
wametakiwa kusimamia Fedha za kuboresha huduma za dharura zinazotolewa
na Serikali zitumike ipasavyo na si kwa matumizi mengine
Hayo yamesemwa na Waziri wa
Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Ummy Mwalimu jijini hapa
wakati akiwa kwenye ziara ya kukagua shughuli za utoaji huduma za afya
pamoja na ujenzi wa huduma za dharura za Uzazi kwenye kituo cha afya cha
Karume kilichopo kata ya Igombe Wilayani Ilemela
Waziri Ummy alimpongeza Mkurugenzi
wa Ilemela kwa matumizi mazuri ya fedha hizo ambapo alijionea kazi
nzuri inayoendelea katika kituo hicho ambapo wametumia wajenzi wa
kawaida na ujenzi huo unaenda vizuri na kwa kiwango kinachoridhisha
Aidha,alisema Fedha za kuboresha
miundombinu ya huduma za uzazi wa dharura zitumike kama haya angalau
kujengwe chumba cha upasuaji,maabara ya damu na tunamataka wodi ya
wazazi na nyumba moja ya mtumishi kuliko kujenga masuala mengine
“kama fedha zitabaki unaweza
kufikiri kujenga vitu vingine,kuliko kqenda kutumika kwa masuala mengine
kama baadhi ya sehemu nyingine wanavyofanya, kama fedha zimebaki nipo
tayari kukuruhusu kujenga kitu kingine Mkurugenzi,hongera sana
Mkurugenzi na viongozi wengine”.
Hata hivyo alisema Tanzania ni
moja ya nchi yenye vifo vingi vya akina mama wajawazito na watoto”leo
hii toka saa sita usiku tuanze siku hadi saa sita usiku wanawake 30 wa
kitanzania wanafariki kwa sababu tu ya kutimiza wajibu wao wa kuleta
kiumbe duniani”
“Kwahiyo Mhe.Rais alichokifanya
kwa kushirikiana na wadau tunaboresha huduma za uzazi zikiwepo za
upasuaji wa kumtoa mtoto tumboni,hivyo tumefurahi kuona hapa zile
zshilingi milioni mia tano zimetumika ipasavyo,binafsi nimedhirika na
kazi iliyofanywa hapa karume hivyo naahidi kuleta fedha kwa ajili ya
kuboresha miundombinu ya kituo cha afya Buzurugwa”alime Waziri Ummy
Wakati huo huo nae naibu Waziri wa
Ardhi,Nyumba na Makazi na Mbunge wa Jimbo la Ilemele Dkt.Angela Mabula
alisema wao kama viongozi watahakikisha fedha zote zitakazoenda kwa
ajili ya afya itatumika ipasavyo na wataisimamia ili kuweza kuboresha
miundombinu ya sekta ya afya
Naye Mkuu wa Mkoa wa Mwanza John
Mongela amewataka wananchi wa Igombe kuendeleza mshikamano
wanaouonyesha ili kuendelea kufanya makubwa zaaidi kwa kujiletea
maendeleo”mchakato wa maendeleo chini ya Jemedari wetu rais Magufunli
ndo kwanza umeanza”.
No comments :
Post a Comment