Meneja
wa Wateja wa Tigo Pesa, Mary Rutta (kulia) akiongea kwa njia ya simu na
moja wa washindi wa promosheni ya Tumia Tigo Pesa na Ushinde
iliyofanyika usiku wa kuamkia mwaka mpya katika ofisi za Tigo ambapo
Lugano Thomas Mlimi wa Dar es salaam, Kulthum Salim Ally wa Ruvuma na
Maria Josef Maligisa wa Lindi walijinyakulia shilingi milioni 15,
milioni 10 na milioni 5 katika promosheni hiyo. Katikati ni Meneja wa
Mapato wa Tigo, Arnold Ngakashi na kushooto ni Mwakilisi wa Bodi ya
Michezo ya Bahati na Sibu Tanzania, Ally Abdallah.
Wateja watatu wajishindia TSH 15 milioni, 10 milioni na 5 milioni!
Dar es Salaam, 31 Desemba, 2017
‘Nimeanza mwaka mpya nikiwa milionea!’ alisema Lugano Thomas Mlini,
ambaye ni dereva na mkaazi wa Mbezi Makonde, jijini Dar es Salaam
alipotaarifiwa kuwa amejishindia shilingi milioni 15 kutoka Tigo.
Kupitia
huduma yake ya Tigo Pesa, kampuni ya simu inayoongoza ya Tigo
imewageuza Watanzania watatu kuwa matajiri wapya kwa mwaka 2018.
‘Ndoto
zangu za kuanzisha biashara sasa zimetimia! Ahsanteni sana Tigo’
alisema Kulthum Salim Ally, mkulima na mkaazi wa Tunduru, Ruvuma ambaye
naye alijinyakulia kitita cha shilinigi 10 milioni katika drooo kabambe
ya promosheni ya Tumia Tigo Pesa na Ushinde iliyofanyika siku ya mkesha
wa kuamkia mwaka mpya, katika ofisi ya makao makuu ya Tigo jijijni Dar
es Salaam.
‘Nilienda
kulala nikiwa maskini na sasa nimeamka nikiwa tajiri’ alisema Mariam
Josef maligisa, Mkulima na mkaazi wa Nagangu, Lindi aliyeamka kutoka
usingizini ili kupokea simu yake na kutaarifiwa kuwa naye amejishindia
TSH 5 milioni kutoka Tigo.
Akitangaza
washindi katika droo hiyo ya kuukaribisha mwaka mpya, Meneja wa Wateja
wa Tigo Pesa, Mary Rutta alisema, ‘Tigo pesa ni zaidi ya huduma ya
kufanya malipo. Ni sehemu ya maisha. Kwa hiyo leo tumewawezesha wateja
wetu kutumiza ndoto zao za msimu wa sikukuu na Mwaka Mpya kupitia huduma
ya Tigo Pesa.
Alibainisha
kuwa Tigo imetoa jumla ya shilingi 120 milioni kwa watu 153 kutoka
maeneo mbali mbali ya nchi. Wateja walishinda zawadi nono za kila siku
baada ya kutumia huduma ya Tigo Pesa.
‘Pia
tunajivunia mchango wetu katika kufanikisha upatikanaji wa huduma za
kifedha nchini. Kupitia Tigo Pesa, tunawawezesha mamilioni ya Watanzania
kutuma na kupokea zaidi ya TSH 1.7 bilioni kila mwezi. Hii inawawezesha
wateja wenyewe pamoja na jamii, huku ikichangia ukuaji wa uchumi wa
nchi,’ aliongeza.
Kwa
upande wake, Kaimu Mkurugenzi wa Huduma za Masoko wa Tigo, Willima
Mpinga alisema kuwa,’Tigo inawatakia Watanzania wote Mwaka Mpya wenye
furaha na mafanikio. Tigo ni mtandao unaowaelewa zaidi wateja na kujibu
mahitaji ya soko. Tulizindua promosheni ya Tumia Tigo Pesa na Ushinde
kwa dhumuni kuu la kuwawezesha wateja wetu kushinda pesa
zitakazowawezesha kutimiza malengo yao ya mwisho mwaka.’
Tigo
Pesa ni huduma ya kifedha kwa njia ya simu ya pili kwa ukubwa nchini.
Tigo Pesa ina mtandao mpana zaidi wa wakala na watoa huduma zaidi ya
70,000 waliosambaa nchini kote. Tigo Pesa pia ilikuwa ndio huduma ya
kwanza Afrika Mashariki iliyowezesha wateja kutuma fedha kwenda nchi
nyingine kwa kutumia viwango na fedha za nchi husika.
Tigo
ndio kampuni inayoongoza kwa mageuzi ya kidigitali ikijivunia huduma
bora za sauti, SMS, intaneti yenye kasi ya juu zaidi ya 4G iliyosambaa
katika miji 24 nchini, pamoja na huduma za kifedha. Mtandao wa Tigo pia
ni maarufu kwa promosheni na ofa zake bunifu kwa wateja.
Tigo
ilianza kutoa huduma zake Tanzania mwaka 1995 na kwa miaka mitatu sasa
ndio kampuni ya simu inayokua kwa kasi zaidi nchini. Kwa sasa Tigo ndio
kampuni ya simu ya pili kwa ukubwa nchini ikiwa na wateja zaidi ya 11.6
milioni.
No comments :
Post a Comment