Monday, January 29, 2018

Tamasha la kuonja mvinyo la kampuni ya TDL 2018 lafana


Kampuni ya TDL maarufu kama Konyagi ambayo ni kampuni tanzu ya TBL Group mwishoni mwa wiki iliandaa tamasha la maonyesho ya kuonja vinywaji vya wine vinavyotengenezwa na kampuni hiyo yenye makao makuu yake jijini Dar es Salaam.
Tamasha hilo lililofanyika katika hoteli ya Southern sun ya jijini Dar es Salaam lilikuwa kivutio kwa watu wengi na waliouhudhuria walipata burudani za kila aina na kutambua na kufurahia ubora wa vinywaji vya kampuni hiyo bila kusahau kucheza muziki,kupata maakuli na kujishindia zawadi mbalimbali.
????????????????????????????????????
Baadhi ya wafanyakazi wa Konyagi katika picha ya pamoja wakati wa tamasha hilo.
????????????????????????????????????
Mtaalamu wa uzalishaji wa Wine ya Dodoma ,Erick Schlunz,  akiwa na mke wake Hcona Schlunz  akitoa maelezo juu ya uzalishaji wa Wine ya Dodoma wakati wa tamasha hilo.
????????????????????????????????????
????????????????????????????????????
Meneja Masoko wa TDL , Warda Kimaro, baadhi ya wananchi waliotembelea banda lao kampuni ya Konyagi.
????????????????????????????????????
????????????????????????????????????
Mwanamuziki wa  Bongo Flava Lady Jay Dee,(kulia) naye alikuwa ndani ya nyumba.
????????????????????????????????????
Meneja Mwandamizi wa TDL,Salvatory Rweyemamu (kushoto) akiojesha mvinyo bora wa kampuni kwa mmoja wa wasnanchi waliotembelea tamasha.
????????????????????????????????????
Mameneja Waandamizi wa kampuni ya TDL wakionyesha aina mbalimbali za mvinyo unaozalishwa na kampuni yao.

No comments :

Post a Comment