Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo
ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akiongea na
wananchi waliofika kupata huduma katika Taasisi ya Mifupa MOI, katika
ziara yake ya kukagua ubora wa huduma za Afya zinazotolewa katika
Taasisi hiyo.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo
ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akikagua Cheti
cha mmoja kati ya wagonjwa waliofika kupata huduma za matibabu katika
Taasisi ya Mifupa ya MOI, katika ziara yake ya kukagua ubora wa huduma
za Afya zinazotolewa katika Taasisi hiyo.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo
ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akifuatilia
idadi ya Dawa katika mfumo wa Kompyuta katika Taasisi ya Mifupa ya MOI.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo
ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akikagua
utunzwaji na uhifadhi wa dawa, katika Taasisi ya Mifupa ya MOI wakati
alipofanya ziara yake ya kukagua ubora wa huduma za Afya zinazotolewa
katika Taasisi hiyo.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo
ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile (Wakwanza)
akiteta jambo na viongozi wa Taasisi ya Mifupa ya MOI wakati alipofanya
ziara yake ya kukagua ubora wa huduma za Afya zinazotolewa katika
Taasisi hiyo, wakatika ni Mkurugenzi wa Taasisi hiyo Dkt. Respicious
Boniface.
…………………………………………………………………………………………………..
Na WAMJWW. DSM
Serikali kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na watoto Taasisi ya Tiba ya Mifupa, Ajali na Upasuaji wa Ubongo na Mishipa ya Fahamu (MOI) shilingi Bilioni 16 ikiwa ni jitihada za Serikali katika kuboresha huduma zinazotolewa na taasisi hiyo kwa
wananchi,Serikali kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na watoto Taasisi ya Tiba ya Mifupa, Ajali na Upasuaji wa Ubongo na Mishipa ya Fahamu (MOI) shilingi Bilioni 16 ikiwa ni jitihada za Serikali katika kuboresha huduma zinazotolewa na taasisi hiyo kwa
Hayo yamesemwa leo na Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya jamii,
Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akiwa katika ziara yake
ya kukagua Ubora wa Huduma zinazotolewa kwa wananchi na taasisi hiyo.
“Serikali imewapa fedha, Bilioni 16 ya kununua vifaa
vyakutumika kwenye jingo lao jipya, watafunga mashine mpya za kisasa
pamoja na CT-Scan na MRI, Thieta pamoja na kufungua kitengo cha zarura
jambo litalopunguza usumbufu kwa wananchi wanaohitaji huduma”, alisema
Dkt. Ndugulile.
Kwa upande mwingine Dkt. Ndugulile ameahidi kuendelea
kushirikiana na Taasisi hiyo katika kuhakikisha wanaiwezesha zaidi ili
kuweza kufanya upasuaji mkubwa ndani ya nchi jambo litakalopunguza
usumbufu kwa mwananchi mwenye kipato cha chini.
Aidha, Dkt. Ndugulile aliupongeza uongozi wa Taasisi ya Moi kwa
kazi kubwa na nzuri wanayoifanya katika kuhakikisha wanatoa huduma bora
za Afya kwa wananchi hali iliyosaidia kupunguza idadi kubwa ya wagonjwa
kwenda nje ya nchi kwaajili ya matibabu ya mifupa.
“Niupongeze uongozi wa Taasisi ya Moi kwa kazi kubwa na nzuri
ambayo wanaendelea kuifanya katika magonjwa yanayohusiana na mifupa
jambo lililosaidia kupunguza wagonjwa wengi sana kupata huduma nje ya
nchi” alisema Dkt. Ndugulile.
Nae Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi hiyo Dkt. Respicious Boniface
amesema kuwa Taasisi hiyo imefanikiwa kwa kiasi kikubwa sana kwani Zaidi
ya Asilimia 95 ya maradhi ya mifupa hutibiwa katika Hospitali hiyo na
asilimia zilizobaki huwapeleka nje ya nchi.
Dkt. Respicious Boniface aliendelea kuishukuru Serikali kwa
Msaada huo wa Fedha kwaajili ya kununua Vifaa vya MRI na CT-Scan na
kuahidi vifaa hivyo vitafika mapema ndani ya mwezi wa Nne, hivyo kazi ya
kuwaudumia wananchi itaanza mapema.
“Sababu kubwa ilikuwa ni vifaa, sasa tayari Serikali kupitia
Wizara ya Afya imekwisha toa fedha kwaajili ya vifaa hivyo hivyo ndani
ya mwezi wa nne vitakuwa vimekwishafika”, alisema Dkt. Dkt. Respicious
Boniface
No comments :
Post a Comment