Rahma
Mwita Abdallah na Paschal Masulu wamechaguliwa kuwawakilisha vijana wa
Tanzania kwenye Baraza la Uchumi na Jamii (ECOSOC) jijini New York.
Wawili hao walichaguliwa kupitia shindano lililoendeshwa na Umoja wa
Mataifa kupitia mitandao ya kijamii ambapo walitakiwa kupakia video ya
dakika moja wakieleza kwanini wachaguliwe kuwawakilisha vijana wa
Tanzania kwenye Baraza la ECOSOC.
Baraza
hilo linakutanisha vijana viongozi kutoka ulimwenguni kwote kujiunga na
waunda sera kujadili changamoto mbalimbali zinazowakumba vijana katika
nchi wanazotoka na jinsi ya kuzitatua. Pia Mkutano huo unatoa fursa kwa
vijana kutoka nchi balimbali kubadilishana ujuzi wa namna ya kutatua
changamoto za vijana katika nchi zao.
Mkutano
huo utafanyika kuanzia Jumatatu ya Januari 30 hadi 31 na unaweza kupata
tarifa za safari ya Rahman na Paschal kwa kufuatilia akaunti za Umoja
wa Mataifa katika Twitter @UnitedNationsTZ na Instagram @unitednationstz
KAWAIDA
Umoja wa Mataifa Tanzania
wachagua vijana watakaoiwakilisha Tanzania kwenye Baraza la Uchumi na
Jamii (ECOSOC) 2018 jijini New York
Rahma Mwita Abdallah na Paschal
Masulu wamechaguliwa kuwawakilisha vijana wa Tanzania kwenye Baraza la
Uchumi na Jamii (ECOSOC) jijini New York. Wawili hao walichaguliwa
kupitia shindano lililoendeshwa na Umoja wa Mataifa kupitia mitandao ya
kijamii ambapo walitakiwa kupakia video ya dakika moja wakieleza kwanini
wachaguliwe kuwawakilisha vijana wa Tanzania kwenye Baraza la ECOSOC.
No comments :
Post a Comment