Subira Kaswaga – NEC
Tume
ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imesema kuwa uchaguzi mdogo katika majimbo
ya Siha mkoani Kilimanjaro na Kinondoni mkoani Dar es Salaam
pamoja na Kata nne za Tanzania Bara utafanyika Februari 17,
2018 kufutia waliokuwa Wabunge katika majimbo hayo kujivua Uanachama na
kukosa sifa za kuendelea kuwa wabunge.
Taarifa
ya Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Jaji Mkuu
Mstaafu wa Zanzibar Hamid Mahmod Hamid imeeleza kuwa pamoja na Majimbo
hayo,pia Kata nne za Isamilo katika Halmashauri ya Wilaya ya
Nyamagana mkoani Mwanza, Manzase Halmashauri ya Wilaya ya
Chamwino mkoani Dodoma, Madanga Halmashauri ya Wilaya ya
Pangani mkoani Tanga na Kimagai Halmashauri ya Wilaya ya
Mpwapwa mkoani Dodoma zitafanya Uchaguzi mdogo
Aidha,
Jaji Mkuu (Mst. Zanzibar) Hamid Mahmoud Hamid amesema kuwa,
Tume inaendesha uchaguzi huo baada ya kupokea barua kutoka kwa
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano Mh. Job Ndugai kuhusu
uwepo wazi wa jimbo la Kinondoni jijini Dar es Salaam na
Jimbo la Siha mkoani Kilimanjaro.
Jaji
Mahmoud amesema kuwa, barua hiyo ilieleza kuwa majimbo hayo
yapo wazi baada Maulid Mtulia aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la
Kinondoni kujivua uanachama wa CUF na Dr. Godwin Mollel wa
jimbo la Siha kujiuzulu uanachama wa CHADEMA na hivyo wote
kukosa sifa za kuwa Wabunge.
Pia,
ameeleza kuwa Tume ilipokea taarifa kutoka kwa Waziri mwenye
dhamana ya Serikali za Mitaa ikiitaarifu Tume uwepo wa nafasi
wazi za Udiwani katika kata nne za Tanzania Bara.
“Baada
ya kupokea barua hizo Tume kwa kuzingatia vifungu vya 37(1)
na 46(2) vya Sheria ya Taifa ya Uchaguzi sura ya 343 pamoja
na kifungu cha 13(3) cha Sheria ya Uchaguzi wa Serikali za
Mitaa sura ya 292 inatangaza kuwa majimbo mawili na kata nne
zipo wazi” alisema Jaji Mahmoud.
Ameeleza
kuwa, fomu za uteuzi kwa majimbo hayo mawili na kata nne
itakuwa kati ya tarehe 14 – 20 Januari, 2018, uteuzi wa
wagombea utafanyika tarehe 20/01/2018, na Kampeni za uchaguzi
mdogo zitafanyika kuanzia tarehe 21/01 – 16/02/2018 na siku ya
uchaguzi itakuwa tarehe 17/02/2017.
Vilevile,
Jaji Mahmoud amevikumbusha Vyama vya Siasa na wadau wote wa
uchaguzi kuzingatia sheria, kanuni, taratibu, miongozo na
maelekezo yote wakati wa uchaguzi huo mdogo.
No comments :
Post a Comment