Tuesday, January 23, 2018

NAIBU WAZIRI WA ELIMU ATAKA VIFAA VYENYE THAMANI YA SH 14 BILIONI VIFUNGWE HARAKA


Naibu Waziri wa Elimu,Sayansi na Teknolojia,William Ole Nasha
akitoa hotuba yake wakati wa mahafali ya tisa ya Chuo cha Ufundi
Arusha(ATC)

Naibu
Waziri wa Elimu,Sayansi na Teknolojia,William Ole Nasha(wa pili kuli)
akiwapongeza wanafunzi wahitimu waliofanya vizuri zaidi katika kozi
walizosomea

Naibu
Waziri wa Elimu,Sayansi na Teknolojia,William Ole Nasha(katikati),Kaimu
Mkuu wa Chuo cha Ufundi
Arusha(ATC),Dk Masudi Senzia(wa pili kulia),Makamu Mkuu wa
Chuo,Utawala,Fedha na Mipango,Dk Erick Mgaya pamoja na viongozi wengine
wakiwa katika picha ya pamoja na wahitimu wasichana.
     
Arusha.Naibu
Waziri wa Elimu,Sayansi na Teknolojia,William Ole Nasha ameuagiza
uongozi wa Chuo cha Ufundi Arusha(ATC) uwe umefunga vifaa vya kisasa
vyenye thamani ya Sh 14 bilioni ndani ya wiki nne badala ya siku 67 ili
vianze kutumika mara moja.
 
Ametoa
agizo hilo kwenye mahafali ya tisa ya wahitimu 465 wa fani mbalimbali
za ufundi jijini hapa  kuwa ukarabati na upanuzi wa karakana ufanyike
ndani ya muda alioutoa ili vifaa hivyo vitumike kwa malengo
yaliyokusudiwa.
 
“Nilipotembelea
Chuo hiki Desemba 2,mwaka jana nilitoa maagizo mharakishe ujenzi na
ukarabati wa miundombinu itakayotumika kufunga vifaa hivyo kutoka
Austria,nafarijika kusikia kuwa utaanza mara moja kwani Wizara ilishatoa
kibali cha kutumia watalaam wenu wa ndani na fedha mnayo,”alisema Ole
Nasha
 
Alisema
sekta ya elimu ya ufundi kwa mujibu wa Dira ya Maendeleo ya Taifa ya
2015 inatarajiwa kuleta maendeleo ya haraka ya rasilimali watu
walioelimika na kupenda kujielimisha zaidi ili kulifanya taifa lipate
maendeleo.
 
Ole
Nasha aliongeza kuwa elimu ya ufundi ina mchango mkubwa katika kufikia
uchumi wa kati unaotegemea viwanda na nchi zilizoendelea kama Japan na
China zimefikia hapo zilipo kwa kutilia mkazo elimu ya ufundi.
 
“Katika
Mpango wa Pili wa Taifa wa Maendeleo 2016/17 hadi 2020/21 tunalenga
kuongeza idadi ya wahitimu wa Vyuo vya Ufundi Stadi(Veta) kutoka 150,000
hadi 700,000  na Vyuo vya Elimu ya Ufundi vinavyotoa elimu ya Kati
kutoka 40,000 hadi 80,000,”alisema
 
Kuhusu
idadi ya wasichana wanaosoma elimu ya ufundi kuwa ndogo alivitaka vyuo
vyote vya ufundi nchini kuweka mikakati ya kuongeza udahili ikiwa ni
pamoja na kutoa kipaumbele maalum kwa kwa wanafunzi wa kike wanaomba
kujiunga.
 
Pia
aliagiza Mamlaka ya Elimu nchini(TEA)kuharakisha upatikanaji wa fedha
kiasi cha Sh 1.7 bilioni kilichotengwa kwaajili ya ujenzi wa hosteli za
wasichana katika Chuo hicho ili kupunguza pengo katika wavulana na
wasichana.
 
Kwa
upande wake Kaimu Mkuu wa Chuo cha ATC,Dk Masudi Senzia alisema
wahitimu 465 wamemaliza katika ngazi za Astashahada ya awali,Astashahada
,Stashahada na Shahada  huku wahitimu wa kike ni 101 sawa na silimia
21  na wahitimu wa kiume  ni 364 sawa na asilimia 78.
 

No comments :

Post a Comment