Mwanzilishi wa Chama cha
Wanamitindo Tanzania (FAT) Mustafa Hassanali (kulia) akifafanua jambo
kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa uzinduzi wa chama
hicho mapema hii leo jijini Dar es Salaam, katikati ni Katibu Mtendaji
toka Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) Godfrey Mngereza na kushoto ni
Mwanamitindo mkongwe nchini Bi. Asia Idarous.
Katibu Mtendaji toka Baraza la
Sanaa la Taifa (BASATA) Godfrey Mngereza (katikati) akizungumza na
waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa uzinduzi wa Chama cha
Wanamitindo Tanzania (FAT) mapema hii leo jijini Dar es Salaam, kulia ni
Rais wa Shirikisho la Sanaa za Ufundi TanzaniaAdrian Nyangamalle na
kushoto ni Mwanamitindo mkongwe nchini Bi. Asia Idarous.
Picha na Idara ya Habari (Maelezo
……………..
BARAZA la Sanaa la Taifa (BASATA)
kwa kushirikiana na wabunifu wa Tanzania wamezindua Chama cha Mitindo
Tanzania (FAT) kitakachowaunganisha wabunifu wote hatua inayolenga
kuinua na kuiongezea hadhi sekta ya mitindo nchini.
Akizungumza na waandishi wa
habari leo Jijini Dar es Salaam Katibu Mtendaji wa Baraza la...
Sanaa la
Taifa (BASATA) Bw. Godfrey Mngereza amesema sekta ya mitindo nchini
ikiimarishwa itaweza kuleta mapinduzi makubwa kwa kuzalisha ajira kwa
vijana.
“Katika kuunga mkono juhudi za
Mheshimiwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli katika kujenga Tanzania ya
viwanda, tasnia ya ubunifu wa mavazi, tumeamua kulima pamba ambayo ndiyo
itakayozalisha mavazi, hivyo kusingekuwa na wabunifu hatungekuwa na
mavazi yenye utamaduni wa Tanzania”
Aidha Mngereza aliongeza kuwa
Tanzania ni miongoni mwa nchi zinazoongoza katika uzalishaji wa ngozi
duniani, ambapo katika kutumia fursa hiyo, Chama cha wabunifu Tanzania
kimepanga raslimali hiyo kwa kuzalisha bidhaa mbalimbali ikiwemo viatu,
mikanda na mabegi .
Naye mwanzilishi wa chama hicho
Bw. Mustafa Hassanali amesema kuwa lengo la kuanzishwa kwa chama hicho
ni katika kukuza, kuimarisha na kuendeleza sekta ya mitindo Tanzania
pamoja na kuwapatia ujuzi, uzoefu wadau wote wa sekta ya mitindo
Tanzania.
Kwa upande wake, Rais wa
Shirikisho la Sanaa za Ufundi Tanzania, Adrian Nyangamalle amekipongeza
chama hicho na kusema kuwa tasnia ya mitindo imetoa ajira kubwa kwa
vijana na kuahidi kuendelea kutoa ushirikiano na jumuiya hiyo ili
kutimiza malengo yake kwa haraka.
Aidha Nyangamalle ameongeza kuwa
Shirirkisho la Chama cha Ufundi kwa kushirikiana na BASATA wameanzisha
mchakato wa kuwatambua wasanii wote nchini kwa kuandaa kanzi data
itakayosaidia kufahamu wasanii waliopo nchini ili kuweza kutambulisha
mchango wao katika kuinua uchumi.
No comments :
Post a Comment