Waziri wa nchi ofisi ya Rais
Selemani Jafo akikagua daraja la Gologombe ambalo limejengwa katika
kata ya mafizi wakati alipofanya ziara yake ya kikazi ya siku moja
Wilayani Kisarawe kwa ajili ya kuweza kutembelea miradi mbali mbali ya
maenedeleo na kujione a changamoto zilizopo.
Waziri Jafo baada ya kutembelea
mradi wa shule ya msingi Mtengwe ambayo kwa sasa inafanyiwa ukarabati wa
baadhi ya madarasa ambayo yalikuwa yapo katika hali mbaya kutokana na
uchakavu wa miundombinu yake.
Waziri wa Nchi ofisi ya Rais
Seleman Jafo wa kulia akitoka kukagua mradi wa bwawa kubwa la
kuhifadhia maji lililopo kata ya Chole ambalo litaweza kuwanufaisha
wakazi wa eneo hilo na maeneo mengine ya jirani kuweza kupata huduma ya
maji.
PICHA ZOTE NA VICTOR MASANGU
…………
NA VICTOR MASANGU, KISARAWE
WAZIRI
wa nchi ofisi ya Rais Tamisemi Selemani Jafo ameahidi kulivalia njuga
suala la baadhi ya wakandarasi hapa nchini ambao ni wazembe na
wanashindwa kutekeleza majukumu yao kwa wakati waliopangiwa ikiwemo
sambamba na watendaji wavivu ambao wanachangia kwa kiasi kikubwa
kukwamisha juhudi za seriklali ya awamu ya tano katika utekelezaji wa
miradi ya maendeleo kwa wananchi na badala yake watachukulia hatua kali
za kisheria ikiwemo kuwafikisha mahakamani.
No comments :
Post a Comment