Waviu Washauri kutoka mkoa wa
Mwanza wametembelea vituo vikubwa vya tiba na matunzo katika hospitali
ya Rufaa ya Bugando na Sekotoure jijini Mwanza ili kujifunza kwa kuona
huduma mbalimbali zinazotolewa katika maeneo hayo.
………………………………………………………………..
Waviu washauri ni watu
wanaoishi na maambukizi ya virusi vya Ukimwi na wamejiweka wazi na huru
kuwashauri watu wanaoishi na VVU kuhusu mambo mbalimbali ya afya ikiwemo
ufuasi mzuri wa dawa, kutoa ushauri nasaha,kufundisha kwa njia ya
ushuhuda wa maisha yao na kuhamasisha Waviu kujiunga katika vikundi ili
kusaidiana na kupunguza unyanyapaa.
Lengo la mafunzo hayo kwa njia
ya matembezi (Field Trip) ni kuwawezesha Waviu washauri kupata ubunifu
wa kuboresha huduma mara watakaporudi kwenye maeneo yao ya kazi.
Miongoni mwa mambo
waliyojifunza katika ziara hiyo iliyofanyika Novemba 30,2017, ni kuhusu
utaratibu mzima wa utunzaji kumbukumbu,mtiririko wa huduma tangu mteja
anapoingia hadi anatoka,njia mbalimbali za kukabiliana na wateja watoro
na wapitaji,utoaji wa elimu sahihi ya VVU na Ukimwi na matumizi sahihi
ya dawa na lishe bora.
Jumla ya Waviu washauri 63
kutoka halmashauri za wilaya za
Ilemela,Kwimba,Magu,Buchosa,Misungwi,Sengerema na Nyamagana wamekutana
jijini Mwanza katika warsha ya siku tatu iliyoanza Novemba 28,2017 hadi
Novemba 30,2017 kwa ajili ya kujengewa uwezo wa namna ya kuboresha
huduma katika vituo vya tiba na matunzo (CTC).
Warsha hiyo iliandaliwa na
Shirika la Ariel Glaser Pediatric Aids Healthcare Initiative (AGPAHI)
linalojihusisha na huduma zinazohusiana na Virusi Vya Ukimwi (VVU) na
UKIMWI katika mikoa ya Shinyanga,Simiyu,Mwanza,Geita,Tanga na Mara kwa
ufadhili wa Watu wa Marekani kupitia shirika la Centres for Disease
Control and Preventation (CDC).
Warsha hiyo imemalizika siku
moja kabla ya siku ya Ukimwi duniani ambayo huadhimishwa kila mwaka
Disemba Mosi na kauli mbiu ya mwaka huu ni ‘Changia mfuko wa udhamini wa kudhibiti Ukimwi nchini uokoe maisha – Tanzania bila Ukimwi inawezekana’.
Kushoto ni Afisa Miradi Huduma
Unganishi kwa jamii AGPAHI mkoa wa Mwanza, Cecilia Yona akitambulisha
Waviu washauri waliotembelea hospitali ya rufaa Bugando jijini Mwanza
kwa ajili ya kujifunza kwa kuona huduma mbalimbali zinazotolewa katika
maeneo hayo. Katikati ni mtoa huduma za afya katika kituo cha tiba na
matunzo katika hospitali ya Rufaa ya Bugando Shija Mashimba. Kulia ni
Muuguzi Kiongozi kitengo tiba na matunzo katika hospitali ya Rufaa ya
Bugando jijini Mwanza, Sarah Bipa.
Muuguzi Kiongozi kitengo tiba
na matunzo katika hospitali ya Rufaa ya Bugando jijini Mwanza, Sarah
Bipa akielezea kuhusu namna wanavyopokea wateja na kuwahudumia.
Muuguzi Kiongozi kitengo tiba
na matunzo katika hospitali ya Rufaa ya Bugando jijini Mwanza, Sarah
Bipa akisalimiana na waratibu wa huduma za afya ngazi ya jamii
walioambatana na Waviu washauri waliotembelea hospitali hiyo.
Sarah Bipa akizungumza na Waviu Washauri waliotembelea hospitali hiyo.
Hapa ni katika eneo la wateja
wanakaa kusubiri huduma: Kulia ni Sarah Bipa akielezea namna
wanavyohudumia wateja,wanavyotoa elimu ya VVU/Ukimwi,elimu ya lishe bora
na ufuasi mzuri wa dawa.
Sarah Bipa akionyesha Waviu washauri namna wanavyotunza mafaili ya wateja katika hospitali hiyo.
Sarah Bipa akiwa na Waviu Washauri katika chumba cha vipimo mbalimbali kama vile uzito na urefu.
Sarah Bipa akiendelea kuwatembeza wageni wake katika maeneo mbalimbali ya hospitali ya rufaa Bugando.
Hapa ni ndani ya chumba cha
ushauri: Pichani ni Muuguzi Mshauri katika hospitali ya Rufaa ya Bugando
jijini Mwanza, Celina Katakomela akielezea namna wanavyotoa elimu kwa
wateja kabla ya kuanza kutumia dawa.
Ndani ya chumba cha dawa : Pichani ni dawa zinazofubaza makali ya VVU.
Waviu washauri wakifuatilia maelezo kutoka kwa Sarah Bipa.
Sarah Bipa akiendelea kuwatembeza wageni wake.
Hapa ni katika hospitali ya
Sekotoure jijini Mwanza: Kulia ni mtoa huduma za afya katika kituo cha
tiba na matunzo hospitali ya Sekotoure,Bernadeta Luhende akionyesha
kitabu cha kutunzia kumbukumbu za wateja.
Mtoa huduma za afya katika
kituo cha tiba na matunzo katika hospitali ya Sekotoure,Heri Abdul
akielezea namna wanavyofuatilia wateja watoro.
Muuguzi Kiongozi katika
hospitali ya Sekotoure jijini Mwanza, Flora Masanja akionesha kitabu kwa
ajili ya kufuatilia wateja watoro.
Muuguzi Kiongozi katika
hospitali ya Sekotoure jijini Mwanza, Flora Masanja akizungumza na Waviu
Washauri.Alisema wastani wa wateja 80 hufika katika hospitali hiyo kila
siku.
Muuguzi Kiongozi katika hospitali ya Sekotoure jijini Mwanza, Flora Masanja akionyesha Waviu namna ya kujaza taarifa za wateja.
Mtoa huduma za afya katika
kituo cha tiba na matunzo katika hospitali ya Sekotoure, Heri Abdul
akionyesha mafaili yanayotumika kutunzia kumbukumbu za wateja wanaofika
katika hospitali hiyo.
Mratibu wa watoa huduma za afya
ngazi ya jamii mkoa wa Mwanza, Bi. Esperance Makuza, aliyemwakilisha
Mratibu wa Ukimwi mkoa wa Mwanza akifunga warsha ya siku tatu ya Waviu
washauri mkoa wa Mwanza katika ukumbi wa JB Belmont Hotel jijini Mwanza
Novemba 30,2017.
Waviu washauri wakimsikiliza Bi. Esperance Makuza wakati akifunga warsha hiyo.
Picha zote na Kadama Malunde – Malunde1 blog
No comments :
Post a Comment