Sunday, December 31, 2017

WATALII WA NJE NA NDANI WAENDELEA KUMIMINIKA HIFADHI YA TAIFA YA SERENGETI


Watalii  wakiwasili  uwanja mdogo wa ndege wa
Seronera wilayani Serengeti mkoa wa Mara uliopo kwenye Hifadhi ya Taifa
ya Serengeti(Senapa) kwaajili ya kutembelea vivutio vya kitalii
wakati wa mapumziko ya mwisho wa mwaka.

Watalii wakiwasili uwanja mdogo wa ndege wa
Seronera wilayani Serengeti mkoa wa Mara ndani ya Hifadhi ya Taifa
ya Serengeti,kukamilika kwa jengo la wageni wanaowasili na wanaondoka kumerahisisha huduma za usafiri ndani ya hifadhi hiyo.

Afisa Utalii Mwandamizi wa Hifadhi ya Taifa Serengeti mkoa
wa Mara,Susuma Kusekwa akizungumza na watalii waliotembelea hifadhi hiyo.

Watalii wakimsikiliza Zacharia Mathayo ambaye ni mwongoza watalii wakati akitoa maelezo kuhusu uhamaji wa
wanayamapori aina ya Nyumbu kutoka Kaskazini mwa Hifadhi ya Taifa Serengeti  hadi Kusini.

Watalii hufurahia kuona wanyama wakubwa wakiwemo Tembo na wengine wanaonekana ndani ya Hifadhi ya Taifa Serengeti.

Tembo ni mojawapo ya kivutio kikubwa kwa watalii wanaotemebela hifadhi hiyo.

Wanyama wadogo aina ya Pimbi ni sehemu ya vivutio utakavyokutana navyo ndani ya Hifadhi ya Taifa ya Serengeti.

Wanyama wadogo aina ya Pimbi ni sehemu ya vivutio utakavyokutana navyo ndani ya Hifadhi ya Taifa ya Serengeti.

Hifadhi
ya Taifa ya Serengeti imefanikiwa kutangaza vivutio vyake kikamilifu
sio kwa watalii wanaotoka  mataifa ya Ulaya,Asia  na Amerika pekee bali
pia watalii wa ndani ni sehemu ya wageni wanaotembelea hifadhi hiyo.
Makundi makubwa ya Simba kama hili utayaona ndani ya hifadhi hiyo.
Serengeti.Idadi ya watalii wanaotembelea Hifadhi ya Taifa
ya Serengeti(Senapa) imeongezeka katika siku za hivi karibuni kutokana na sekta
ya utalii kukua huku miundombinu ya barabara na viwanja vidogo vya ndege
vilivyopo ndani ya hifadhi hiyo kufanya kazi vizuri.
 
Afisa Utalii wa Senapa,Evance Magomba alisema kuwa
baada ya kujengwa jengo dogo la wageni wanaowasili na wanaoondoka katika uwanja
mdogo wa ndege wa Seronera idadi ya wageni imeongezeka huku wakala wa makampuni
ya ndege wakiweka wawakilishi wao katika uwanja huo.
 
Kwa mujibu wa takwimu zilizokusanywa katika kipindi cha
Januari hadi Septemba mwaka huu kumekua na safari za ndege 3,724 katika uwanja
wa Seronera huku uwanja wa Lobo katika kipindi hicho ni safari 349 na uwanja wa
Kogatende safari 564.
 
Alisema ndani ya hifadhi hiyo kuna viwanja vidogo vya
ndege saba kikiwemo cha  Seronera ambacho
ni kikubwa zaidi chenye uwezo wa kupokea ndege
kubwa yenye uwezo wa kubeba abiria 60 ikiwemo ya shirika la Precision
Air inayofanya kazi mara nne kwa wiki.
 
“Miaka miwili iliyopita hatukua na jengo hili la abiria naamini pamoja na sababu nyingine limekua kishawishi
kwa wageni kuongezeka kwani linawawezesha kuwa na sehemu
nzuri ya kupumzika kabla ya kuanza safari zao,”alisema Magomba
 
Alisema kutokana na ukubwa wa hifadhi hiyo wanavyo
viwanja vingine vilivyosambaa maeneo mbalimbali ili kutoa huduma kwa urahisi na
kuwawezesha watalii kupata muda mzuri wa kutembelea vivutio zaidi.
 
Magomba alivitaja viwanja vingine kuwa ni
Kogatenda,Lobo,Ndutu,Kirawira ,Fort Ikoma na Lamai ambavyo hutumika kwa malengo
ya kurahisisha kufika eneo husika na kulingana na watalii wanapenda kuona
vivutio maalumu.
 
“Hifadhi ya Serengeti ina uwezo wa kupokea wageni wa aina
zote na zipo huduma za malazi zikiwemo hoteli saba,makambi ya kudumu sita na
makambi ya muda  zaidi 140 yaliyosambaa
na kipekee tuwakaribishe wananchi kutembelea hifadhi zetu kwasababu zipo bei
maalumu kwaajili yao,”alisema Magomba
 
Dereva wa kampuni ya kitalii ya Micato
Safaris,Emmanuel Lema alisema huduma za kitaalii nchi zimekua kwa kasi baada ya
serikali kupitia Bodi ya Utalii(TTB),shirika la Hifadhi za Taifa(Tanapa) na
wadau wengine wa utalii kutangaza kwa kiwango kikubwa sekta ya utalii.
 
Alishauri Tanapa kuongeza ukubwa wa jengo la wanaowasili
na kuondoka na huduma zingine muhimu ili kuwawezesha watumiaji wa jengo hilo
kupata huduma za kiwango cha juu hasa wakati wa msimu wa utalii.
 
Imeandaliwa na www.rweyemamuinfo.blogspot.com

No comments :

Post a Comment