Kaimu Mkurugenzi Idara ya
Maendeleo ya Sanaa Bibi. Leah Kihimbi (wapili kushoto) akizungumza
wakati Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Harrison
Mwakyembe (wapili kulia) alipokutana na wadau wa sekta anazozisimamia
kuhamasisha wadau hao kuunga mkono kampeni ya uzalendo itakayozinduliwa
na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli
tarehe nane Desemba Mkoani Dodoma. Kushoto ni Naibu Waziri wa Habari
Mhe. Juliana
Naibu Waziri wa Habari Utamaduni
Sanaa na Michezo Mhe. Juliana Shonza akizungumza wakati Waziri wa Habari
Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Harrison Mwakyembe alipokutana na wadau
wa sekta anazozisimamia kuhamasisha wadau hao kuunga mkono kampeni ya
uzalendo itakayozinduliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli tarehe nane Desemba Mkoani Dodoma.
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa
na Michezo Mhe. Harrison Mwakyembe akizungumza alipokutana na wadau wa
sekta anazozisimamia kuhamasisha wadau hao kuunga mkono kampeni ya
uzalendo itakayozinduliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli tarehe nane Desemba Mkoani Dodoma leo
Jijini Dar es Salaam.
Naibu Waziri wa Habari Utamaduni
Sanaa na Michezo Mhe. Juliana Shonza (kulia) pamoja na Mkurugenzi
Maendeleo ya Michezo Bw. Yusuph Singo (katikati) na Katibu Mtendaji Bodi
ya Filamu Bibi. Joyce Fissoo (kushoto) wakifuatilia wakati Waziri wa
Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Harrison Mwakyembe (hayupo
pichani) alipokutana na wadau wa sekta anazozisimamia kuhamasisha wadau
hao kuunga mkono kampeni ya uzalendo itakayozinduliwa na Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli tarehe nane
Desemba Mkoani Dodoma.
Mjumbe wa kamati ya uzalendo Bw.
Mrisho Mpoto (kulia) akizungumza wakati Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa
na Michezo Mhe. Harrison Mwakyembe (katikati waliokaa) alipokutana na
wadau wa sekta anazozisimamia kuhamasisha wadau hao kuunga mkono kampeni
ya uzalendo itakayozinduliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli tarehe nane Desemba Mkoani Dodoma. Wapili
kushoto ni Naibu Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe.
Juliana Shonza
Mwanamziki mkongwe nchini Bw.
John Kitime (aliyesimama) akichangia wakati Waziri wa Habari Utamaduni
Sanaa na Michezo Mhe. Harrison Mwakyembe (hayupo pichani) alipokutana na
wadau wa sekta anazozisimamia kuhamasisha wadau hao kuunga mkono
kampeni ya uzalendo itakayozinduliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli tarehe nane Desemba Mkoani
Dodoma.
Baadhi ya wadau wa sekta za
Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo wakifuatilia matukio mbalimbali
yaliyokua yakiendelea wakati Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo
Mhe. Harrison Mwakyembe (hayupo pichani) alipokutana na wadau wa sekta
anazozisimamia kuhamasisha wadau hao kuunga mkono kampeni ya uzalendo
itakayozinduliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt.
John Pombe Magufuli tarehe nane Desemba Mkoani Dodoma.
Naibu Waziri wa Habari Utamaduni
Sanaa na Michezo Mhe. Juliana Shonza (kushoto) akimkabidhi mshindi wa
shindano la Ubingwa wa Dunia uzito wa kati Bw. Ibrahim Class hundi ya
shilingi milioni kumi na nane wakati Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na
Michezo Mhe. Harrison Mwakyembe (hayupo pichani) alipokutana na wadau
wa sekta anazozisimamia kuhamasisha wadau hao kuunga mkono kampeni ya
uzalendo itakayozinduliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli tarehe nane Desemba Mkoani Dodoma.
Kikundi cha ngoma kikitumbuiza
wakati Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Harrison
Mwakyembe (hayupo pichani) alipokutana na wadau wa sekta anazozisimamia
kuhamasisha wadau hao kuunga mkono kampeni ya uzalendo itakayozinduliwa
na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli
tarehe nane Desemba Mkoani Dodoma.
Picha na: Genofeva Matemu – WHUSM
………………
Na Shamimu Nyaki – WHUSM.
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa
na Michezo Mhe. Dkt Harrison Mwakyembe amewataka Watanzania wote
kujitokeza katika Uzinduzi wa Kampeni ya kitaifa ya Uzalendo
inayotarajiwa kuzinduliwa tarehe 08 Desemba 2017 mjini Dodoma na Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt John Pombe Magufuli.
Akizungumza na Waandishi wa Habari
leo Jijini Dar es Salaam Mhe. Mwakyembe amesema kuwa Wizara yake
imeamua kuanzisha Kampeni ya Uzalendo ili kuwakumbusha watanzania
kupenda,kujali na kuthamini nchi yao kwa kuenzi na kuupenda Utamaduni wa
Taifa letu ambao ndio unaounganisha na kutambulisha watanzania.
“Uzalendo wetu umetikisika ni
lazima sasa kuamka na kujua kuwa tuna jukumu la kuenzi Uzalendo
tuliojengewa na Waasisi wa Taifa letu wa kupenda nchi yetu na kudumisha
Utamaduni wetu”Alisema Mhe. Waziri Mwakyembe.
Aidha amewataka watanzania pia
kutumia lugha ya Kiswahili kwa ufasaha katika maisha ya kila siku kwa
kuwa Lugha hiyo ndio inayotambulisha Mtanzania popote anapokuwa pamoja
na kuheshimu alama zote za Taifa ikiwemo Bendera ambapo ameagiza
matumizi sahihi ya Bendera hiyo.
Kwa upande wake Naibu Waziri wa
Wizara hiyo Mhe. Juliana Shonza amesema Kampeni hiyo ni muhimu sana kwa
Taifa letu kwakua inalenga kukumbusha jamii Utamaduni wetu ambao ndio
unafanya jamii kuwa na uzalendo katika nyanja zote za maendeleo.
“Ili kufikia adhma ya Serikali ya
awamu ya Tano ya Tanzania ya Viwanda bila kuwa na uzalendo wa kufanya
kazi kwa bidii na kwa kushirikiana.” Alisema Mhe. Juliana.
Mhe. Juliana ameongeza kuwa
Wasanii wanahabari na wanamichezo wanajukumu kubwa sana la kuutangaza
Kampeni hii lakini pia kuelimisha jamii maana ya Uzalendo pamoja na kuwa
mstari wa mbele katika kutenda mambo mazuri yanayoendana na Utamaduni
wa Tanzania kwa wao ni kioo cha jamii.
Naye msanii Mrisho Mpoto ameiahidi
Serikali kushirikiana nayo katika kuelimisha jamii maana ya uzalendo
kupitia sanaa yake ambapo amesema atashirikiana na wasanii wenzake
kuandaa nyimbo zitakazowakumbusha watanzania umuhimu wa Uzalendo ili
kuwa na Taifa lenye jamii inayotambua maana ya uzalendo kama ilivyokuwa
enzi za mababu zetu.
Kampeni ya uzalendo yenye Kauli
mbiu “UZALENDO NA UTAIFA,NCHI YANGU KWANZA” ina lengo la kurejesha hali
ya watu kupenda nchi yao kupinga mmomonyoko wa maadili kwa viongozi wa
Umma,kuongezeka kwa tuhuma za rushwa,kuibuka kwa ufisadi,matumizi mabaya
ya mamlaka na ubaguzi wa aina yeyote ambapo itakuwa inaadhimishwa kila
mwaka.
No comments :
Post a Comment