MWENYEKITI wa kamati ya ulinzi na
usalama mkoani Pwani, ambae pia ni mkuu wa Mkoa huo, mhandisi Evarist
Ndikilo ,akionyesha picha zinazoonyesha korosho zilizochanganywa mawe na
mchanga ,na kusababisha kutia doa minada ya Korosho inayoendelea mkoani
hapo ,wakati alipokuwa wilayani Mkuranga
MWENYEKITI wa kamati ya ulinzi na
usalama mkoani Pwani, ambae pia ni mkuu wa Mkoa huo, mhandisi Evarist
Ndikilo , akizungumza na baadhi ya wakulima wa korosho wakati
alipotembelea ghala moja lililopo wilayani Mkuranga.
Picha na Mwamvua Mwinyi
…………..
Na Mwamvua Mwinyi,Bagamoyo
MWENYEKITI wa kamati
ya ulinzi na usalama mkoani Pwani ,mhandisi Evarist Ndikilo ameliagiza
jeshi la polisi mkoani hapo ,kuwakamatana na kuwahoji viongozi wa vyama
vya ushirika vya msingi (AMCOS)kumi ,kutokana na kosa la kufanya
udanganyifu wa ubora na uzito wa korosho ili kujipatia fedha .
Amesema kuna baadhi
ya AMCOS zimehusika kuchakachua na kutelemsha ubora wa korosho pamoja na
kuweka mawe na michanga kwenye magunia ya korosho zilizokuwa zinauzwa
kwenye minada .
Aidha mhandisi
Ndikilo ,amekemea maghala ya vichochoroni na majumbani ambayo yamejaa na
kusababisha kuchafua na kuharibu minada inayofanyika mkoani Pwani.
Akizungumza wilayani
Mkuranga ,wakati akizungumzia kero hiyo iliyojitokeza alieleza,viongozi
wa AMCOS hizo wakiwemo wenyeviti wake ,makatibu,kalani na wenye ghala
wakamatwe na kueleza kiini cha kutelemsha ubora.
Alisema lifunguliwe
jalada la uchunguzi wahojiwe mazingira na kiini cha kubadili ubora
kutoka kiwango kinachohitajika na kushusha kiwango cha chini.
Mhandisi Ndikilo, alisema biashara hiyo haitaki kwani imesababisha wakulima wa korosho kushindwa kulipwa fedha zao.
“Kuna hii Mchukwi A
-Amcos Two ambayo imechakachua korosho kutoka grade 52 hadi 45.1
,Misugusugu wameshusha kiwango na kufikia 43,Mchukwi A -Amcos One
,Kibaoni ,Ruaruke ,Mahege,Mlanzi na Tuamke hawa wote wamejipanga kabisa
,maana haiwezekani viwe vyama vya msingi kumi huu ni mpango ,haikubaliki
,jamani haikubaliki” alisisitiza .
Akitoa maagizo
mengine manne ,mhandisi Ndikilo alitaka wanunuzi walioshinda mnada na
kushindwa kuwalipa wakulima fedha zao wakamatwe .
“Wapo wanunuzi
walioenda nje ya masharti ya mnada wanapaswa walipe fedha za wakulima
ndani ya siku nne” alisema mhandisi Ndikilo.
Mhandisi Ndikilo
ambae pia ni mkuu wa Mkoa huo ,aliagiza pia makampuni yaliyoshinda na
kutolipa wakulima yakamatwe ama yahakikishe yanalipa ndani ya siku moja.
Alisema, AMCOS ya
Mkiu viongozi wake wakamatwe na kufikishwa mahakamani kwa kuweka mawe na
mchanga kwenye magunia na kuchanganya na korosho.
Alibainisha huo ni
wizi,uhujumu uchumi na kuaibisha sifa ya nchi ya Tanzania nje ya nchi
kwani magunia hayo yangefika India na nchi nyingine ingekuwa aibu na
fedheha.
Mhandisi Ndikilo
alisema kero hizo zilisababisha Mkoa kuchukua hatua ya kufanya uhakiki
upya wa korosho ili kuaminika kwa wanunuzi ambao baadhi yao waligomea
kuingia kwenye soko la korosho mkoani humo .
“Amcos zote nazipa
salamu zijiandae ,zile Amcos zinazong’ang’ania kutumia maghala ya
vichochoroni ili kudhurumu wakulima ,;:”‘. Watie akilini msimu ujao
2018/2019 hawatatumia maghala ya majumbani yatatumika maghala makubwa
matatu likiwemo la Mkuranga, , Kibiti na Kwamfipa Kibaha.”
Alisema ghala la
Mkuranga litakuwa na uwezo wa kubeba korosho tani 30,000 hivyo aliomba
kuondoka katika maghala yasiyo na kichwa wala miguu.
Naibu waziri wa
mifugo na uvuvi ambae pia ni mbunge wa jimbo la Mkuranga, Abdallah Ulega
alisema watu wachache wenye uroho wa fedha na wasio waaminifu wanataka
kuharibu biashara hiyo na kuumiza wakulima.
Alisema kuweka michanga na mawe kwenye korosho imerudisha nyuma minada inayoendelea .
Ulega alisema kuwepo
kwa maghala makubwa itainua soko la korosho msimu ujao na kuondoa
ubabaishaji wa maghala madogomadogo yanayoleta dosari .
Mbunge huyo
,aliupongeza uongozi huo wa Mkoa kuingilia kati na kuchukua hatua ili
kukomesha wizi unaofanywa na baadhi ya vyama vya msingi vya ushirika
vinavyoondoa uaminifu .
Nae Mwenyekiti wa
halmashauri ya Mkuranga, Juma Abeid alisema mfumo wa stakabadhi ghalani
unaharibiwa na baadhi ya watu na kusababisha wakulima kuona mfumo huo
hauna manufaa kwao .
Alisema kuna ujanja mwingi kwenye kuchakachua ubora wa korosho ndio uliowafikisha walipofikia sasa .
Abeid alisema korosho
zipo hadi kwenye nyumba za watu ,kuna maghala Mkuranga zaidi ya 60
,hivyo ni lazima maghala makubwa yakawepo ili kuondokana na kero
zinazojitokeza.
Licha ya minada hiyo
ya korosho kuingia kizungumkuti lakini tayari zaidi ya tani 19,815
zimeuzwa na kuingiza kiasi cha sh.bilioni 39 huku wakulima wakulima wa
korosho mkoani Pwani wakiwa bado wanadai zaidi ya bilioni tano .
No comments :
Post a Comment