Bibi Prisca Mwingira ambaye
alifanyiwa upasuaji wa kupandikizwa figo Novemba 21, mwaka huu
akiishukuru Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), madaktari bingwa wa
hospitali hiyo pamoja na Rais John Pombe Magufuli baada ya afya yake
kuendelea vizuri. Bibi Prisca ameruhusiwa kurejea nyumbani leo saa 6:00
mchana baada madaktari bingwa wa magonjwa figo kufanikisha upasuaji huo
wa kihistoria. Kulia ni Bathelomayo Mwingira ambaye amempatia dada yake
figo. Kushoto ni Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Figo, Dkt. Jacqueline
Shoo, Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Figo Dkt. Kisanga (katikati), wote
wa Muhimbili.
Bibi Prisca Mwingira akimshukuru
kaka yake, Bathelomayo Mwingira kwa kumpatia figo kutokana na tatizo
hilo kumsumbua katika kipindi cha mwaka mmoja.
Baadhi ya waandishi wa habari
kutoka vyombo mbalimbali nchini wakishudia tukio hilo lakihistoria
ambalo limefanywa na madaktari bingwa wa Muhimbili.
Daktari Bingwa wa Magonjwa ya
Figo, Dkt. Jacqueline Shoo akizungumza na waandishi wa habari baada ya
Bibi Prisca kuruhusiwa kurejea nyumbani kutokana na afya yake kuendelea
vizuri.
Baadhi ya wananchi wakishudia tukio hilo leo katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH).
Mzazi wa Bibi Prisca, Mzee
Mwingira akiwashukuru madaktari wa hospitali hiyo kwa kufanikisha
upasuaji huo na sasa mtoto wake anaendelea vizuri kiafya.
Picha na John Stephen, Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH)
………….
Dar
es salaam, Tanzania. Mgonjwa aliyefanyiwa upasuaji wa kihistoria wa
kupandikizwa figo leo ameruhusiwa kutoka katika hospitalini akiwa na
afya njema.
Bibi
Prisca Mwingira ambaye amefanyiwa upasuaji mkubwa na wa kwanza
kufanyika hapa nchini alipandikizwa figo Novemba 21, mwaka huu katika
Hospitali ya...
Taifa Muhimbili (MNH) chini ya timu ya wataalam wa MNH kwa
kushirikiana na watalaam wa Hospitali ya BLK ya nchini India.
Akizungumza
na waandishi wa habari leo baada ya kuruhusiwa kutoka hospitalini Bibi
Prisca amewashukuru watalaamu wote walioshiriki katika kumuhudumia na
pia ametumia fursa huyo kumuomba Rais John Magufulu kuendelea kuisaidia
MNH ili kuhakikisha huduma za kibingwa wa juu zinaendelea kutolewa
katika hospitali hiyo.
“Kipekee
namshukuru mwenyezi Mungu, madaktari , wauguzi, uongozi wa Hospitali ya
Muhimbili pamoja na serikali kwa kufanisha matibabu yangu,
nilisumbuliwa na ugonjwa wa figo takribani mwaka mzima na kuingia katika
matibabu ya kuchuja damu, lakini hatimaye leo kaka yangu amejitolea
figo yake moja na nimewekewa mimi kwa kweli namshukuru sana.
“Napenda
kuwashauri wagonjwa wenye matatizo ya figo na wanaoendelea na huduma ya
kuchuja damu wasikake tamaa kwani sasa matibabu yamepatikana na mimi ni
shuhuda katika hili,’’ amesema Bibi Prisca.
Kwa
upande wake, Bwan Bathelomayo Mwingira ambaye amemtolea figo dada yake,
amesema anafuraha kwani amesaidia kufanikisha matibabu ya dada yake na
anamuomba Mungu afya ya dada yake izidi kuimarika.
Pia,
Baba mdogo wa Prisca , Ainhard Mwingira ameishukuru serikali ya awamu
ya tano kwa kufanikisha huduma za kibingwa kutolewa Muhimbili.
Naye
Daktari Bingwa wa Magonjwa ya figo, Dkt. Jackline Shoo wa Muhimbili
amesema upasuaji wa kupandikiza figo ulitumia takribani saa nne na zoezi
hilo limekamilika vizuri na mgonjwa anarejea nyumbani huku afya yake
ikiwa salama.
“Mgonjwa
anaondoka Hospitalini akiwa mzima salama kabisa , anaenda kujumuika na
familia yake ataishi kama binadamu wengine ingawa kuna masharti
atatakiwa kuyafuata kama alivyoshauriwa na wataalam,” amesema Dkt.
Shoo.
Pia,
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Hudma kwa Wateja, Aminiel Aligaesha
amesema upasuaji huo umegharimu Shilingi Milioni 21 na endapo mgonjwa
angepelekwa nchini India matibabu yake yangegharimu Shilingi Milioni 80
hadi Shilingi milioni 100.
“Kwa
niaba ya uongozi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili nawapongeza watalaam
wote walioshiriki katika upasuaji huu mkubwa na wa kihistoria na pia
naishukuru serikali kwa kufanikisha zoezi hili,’’ amesema.
No comments :
Post a Comment