Goli la shuti kali la Roberto
Firmino limeisaidia Liverpool kutoa sare katika mchezo mzuri wa Ligi
Kuu ya Uingereza ulioshuhudia Arsenal ikifunga magoli matatu ndani ya
dakika tano za kipindi cha pili.
Arsenal ilikuwa nyuma kwa magoli 2-0
yaliyofungwa na Philippe Coutinho aliyefunga goli la kwanza kwa mpira
wa kichwa kabla ya raia wa Misri Mohamed Salah kuongeza goli la pili
katika kipindi cha pili.
Lakini hafla Arsenal walizinduka na
kufunga goli la kwanza kupitia kwa Alexis Sanchez akifunga kwa mpira
wa kichwa krosi ya Hector Bellerin, kabla ya Granit Xhaka kutumbukiza
la pili kisha Mesuit Ozil kufunga la tatu.
Philippe
Coutinho akifunga goli kwa mpira wa kichwa hii ikiwa ni mara ya kwanza
kwa mchezaji huyo kufunga goli kwa mpira wa kichwa katika Ligi Kuu ya
Uingereza
Mohamed Salah akifunga goli la pili la Liverpool kwa shuti lililomshinda kipa wa Arsenal
Alexis Sanchez akiifungia Arsenal goli la kwanza lililoamsha ari ya kusawazisha magoli waliyofungwa na kuongeza moja
Roberto Firmino akiisawazishia Liverpool goli la tatu na kufanya mchezo huo kumalizika kwa sare ya magoli 3-3
No comments :
Post a Comment