Naibu
Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga (kushoto) na Mkuu wa
Wilaya ya Makete, Veronika Kessy wakiangalia maua ya asili ambayo ni
kivutio kikubwa cha utalii katika hifadhi ya Taifa ya Kitulo wakati wa
ziara yake ya kikazi ya kukagua shughuli za uhifadhi na utalii katika
hifadhi hiyo kwenye wilaya ya Makete mkoani Njombe leo. Hifadhi hiyo ni
maarufu duniani kwa kuwa na aina za maua zaidi ya 35 ya asili ambayo
hayapatikani kwengineko duniani. Hifadhi hiyo ni maarufu kwa wenyeji
kama ‘BUSTANI YA MUNGU’.
Naibu
Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga (kushoto), Mkuu wa Wilaya
ya Makete, Veronika Kessy (kulia) na baadhi ya viongozi wa Hifadhi ya
Taifa ya Kitulo wakiangalia maua ya asili ambayo ni kivutio kikubwa cha
utalii katika hifadhi hiyo wakati wa ziara yake ya kikazi ya kukagua
shughuli za uhifadhi na utalii katika hifadhi hiyo kwenye wilaya ya
Makete mkoani Njombe leo. Hifadhi hiyo ni maarufu duniani kwa kuwa na
aina za maua zaidi ya 35 ya asili ambayo hayapatikani kwengineko
duniani.
Naibu
Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga (wa nne kulia), akiwa
kwenye picha ya pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Makete, Veronika Kessy (wa
tatu kulia) na baadhi ya viongozi wa Hifadhi ya Taifa ya Kitulo wakati
wa ziara yake ya kikazi ya kukagua shughuli za uhifadhi na utalii katika
hifadhi hiyo kwenye wilaya ya Makete mkoani Njombe leo. Hifadhi hiyo ni
maarufu duniani kwa kuwa na aina za maua zaidi ya 35 ya asili ambayo
hayapatikani kwengineko duniani.
Naibu
Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga (kulia), Mkuu wa Wilaya
ya Makete, Veronika Kessy na Mhifadhi Mkuu wa Hifadhi ya Taifa Kitulo,
Pius Mzimbe wakiangalia maporomoko ya maji ya Mwakipembo ambayo ni
kivutio cha utalii ndani ya hifadhi ya Kitulo wakati wa ziara ya kikazi
ya kukagua shughuli za uhifadhi na utalii katika hifadhi hiyo kwenye
wilaya ya Makete mkoani Njombe leo. Pamoja na kivutio hicho hifadhi hiyo
ni maarufu duniani kwa kuwa na aina za maua zaidi ya 35 ya asili ambayo
hayapatikani kwengineko duniani. Hifadhi hiyo ni maarufu kwa wenyeji kama ‘BUSTANI YA MUNGU’.
Naibu
Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga (kulia) akipata maelezo
kuhusu maporomoko ya maji ya Mwakipembo ambayo ni kivutio cha utalii
ndani ya hifadhi ya Taifa ya Kitulo kutoka kwa Mhifadhi Mkuu wa Hifadhi
hiyo, Pius Mzimbe wakati wa ziara yake ya kikazi ya kukagua shughuli za
uhifadhi na utalii katika hifadhi hiyo kwenye wilaya ya Makete mkoani
Njombe leo. Kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Makete, Veronika Kessy. Pamoja na
kivutio hicho hifadhi hiyo ni maarufu duniani kwa kuwa na aina za maua
zaidi ya 35 ya asili ambayo hayapatikani kwengineko duniani.
Muonekano mwanana wa Hifadhi
ya Taifa ya Kitulo. Hifadhi hii ina aina zaidi ya 350 za maua huku aina
35 yakiwa ndwele na hupatikana katika hifadhi hiyo pekee duniani.
Vivutio vingine vinavyopatikana katika hifadhi hiyo ni Maporomoko ya
maji, ndege aina mbalimbali ambao wengine huama kutoka ulaya wakati wa
baridi, wanyamapori aina Swala, Mbega na Nsya. Hata hivyo katika
kutimiza mkakati wa Wizara kuboresha vivutio vya utalii, hifadhi hiyo
ipo katika maandalizi ya kuanzisha makazi ya Pundamilia na wanyama
wengine. Awamu ya kwanza ya kuhamisha pundamiliz 25 kutoka hifadhi ya
taifa ya mikumi inatarajiwa kukamilika mwishoni mw mwaka huu. Hifadhi hiyo ni maarufu kwa wenyeji kama ‘BUSTANI YA MUNGU’.
Aina mojawapo ya ua ambalo hupatikana katika hifadhi hiyo.
Mhifadhi
Mkuu wa Hifadhi ya Taifa ya Kitulo, Pius Mzimbe (kushoto) akimuonyesha
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Japhet Hasunga (kulia) sehemu
ya eneo lililochaguliwa ndani ya hifadhi hiyo kwa ajili ya kuanzisha
makazi ya Pundamilia 25 watakaohamishwa kutoka Hifadhi ya Taifa ya
Mikumi. Alisema kabla ya mwaka huu kuisha Pundamilia hao watakuwa
wameshahamishiwa eneo hilo. Huo ni mkakati wa wizara na Serikali katika
kuboresha vivutio vya utalii nchini ili kuongeza idadi ya watalii na
mapato.
Naibu
Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga akisalimiana na
wafanyakazi wa Hifadhi ya Taifa ya Kitulo alipowasili makao makuu ya
hifadhi hiyo yaliyopo Makete mkoani Njombe jana.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga akizungumza na wafanyakazi wa Hifadhi
ya Taifa ya Kitulo makao makuu ya hifadhi hiyo yaliyopo Makete mkoani
Njombe. Amewaaka watumishi hao kufanya kazi kwa bidii na ubunifu,
kujiepusha na vitendo vya rusha, kuweka mikakati wa kudhibiti mifugo
kuingia hifadhini na sio kusubiri iingie na kuanza kutangaza kuikamata
au kuitaifisha, kupunguza malalamiko ya wananchi jirani na hifadhi hiyo,
kuongeza idadi ya mapato ya hifadhi na kufanya kazi kwa kuzingatia
maadili ya utumishi wa umma.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga akizungumza na wafanyakazi wa Hifadhi ya Taifa ya Kitulo. (Picha na Hamza Temba-Wizara ya Maliasili na Utalii)
No comments :
Post a Comment