Naibu
Waziri wa Nchi-Ofisi ya Waziri Mkuu( Kazi,Vijana na Ajira) Anthony
Mavunde akisalimiana na viongozi mbalimbali alipokuwa akifunga mafunzo
ya Ulinzi shirikishi yaliyoshirikisha Vijana 75 katika kata ya
Mtumba,Manispaa ya Dodoma.
NAIBU Waziri wa Nchi-Ofisi ya Waziri
Mkuu( Kazi,Vijana na Ajira) Anthony Mavunde amewataka Vijana ambao wanashiriki
katika mafunzo ya Ulinzi shirikishi kupitia Polisi Jamii kuunda vikundi vya
uzalishaji mali ili kujikwamua kiuchumi na kuongeza kipato.
Mavunde ameyasema hayo leo wakati
akifunga mafunzo ya Ulinzi shirikishi yaliyoshirikisha Vijana 75 katika kata ya
Mtumba,Manispaa ya Dodoma.
“Pamoja na jukumu kubwa mlilonalo na
ulinzi na usalama wa raia na mali zao,lakini pia mhakikishe mnatumia mkusanyiko
wenu kuunda vikundi vya uzalishaji mali ili kujiongezea kipato na kutengeneza
nafasi za Ajira zaidi,”amesema
Mavunde amewataka vijana hao kuyatumia
vyema mafunzo waliyopata kwa kuwa waadlifu,waaminifu na wazalendo kwa Taifa lao
na kusimama mstari wa mbele kuhakikisha Taifa hili linaendelea kuwa na AMANI na
UTULIVU.
Naye, Kamanda wa Mkoa wa Polisi wa
Dodoma,SACP Gilles Muroto amewataka Vijana zaidi kujitokeza katika Ulinzi
shirikishi ili kuimarisha usalama na amani katika mkoa wa Dodoma.
Naibu
Waziri wa Nchi-Ofisi ya Waziri Mkuu( Kazi,Vijana na Ajira) Anthony
Mavunde akipokea heshima kutoka kwa askari polisi katika ufungaji wa
mafunzo ya Ulinzi shirikishi yaliyoshirikisha Vijana 75 katika kata ya
Mtumba,Manispaa ya Dodoma
Naibu
Waziri wa Nchi-Ofisi ya Waziri Mkuu( Kazi,Vijana na Ajira) Anthony
Mavunde akiwa na Kamanda wa polisi Dodoma Gilles Murotop wakikagua
gwaride katika ufungaji wa mafunzo ya Ulinzi shirikishi yaliyoshirikisha
Vijana 75 katika kata ya Mtumba,Manispaa ya Dodoma.
Vikundi vya Ulinzi shirikishi
Naibu
Waziri wa Nchi-Ofisi ya Waziri Mkuu( Kazi,Vijana na Ajira) Anthony
Mavunde akiwa na Kamanda wa Polisi Dodoma Gilles Muroto katika hafla ya
ufungaji wa mafunzo ya Ulinzi shirikishi yaliyoshirikisha Vijana 75
katika kata ya Mtumba,Manispaa ya Dodoma
Naibu
Waziri wa Nchi-Ofisi ya Waziri Mkuu( Kazi,Vijana na Ajira) Anthony
Mavunde akitoa cheti kwa mmoja wa washiriki wa mafunzo ya Ulinzi
shirikishi yaliyoshirikisha Vijana 75 katika kata ya Mtumba,Manispaa ya
Dodoma
Naibu Waziri wa Nchi-Ofisi ya Waziri Mkuu( Kazi,Vijana na Ajira) Anthony Mavunde akimvisha utambulisho mmoja wa washiriki wa mafunzo ya Ulinzi shirikishi yaliyoshirikisha Vijana 75 katika kata ya Mtumba,Manispaa ya Dodoma
No comments :
Post a Comment