Friday, December 1, 2017

MATUKIO MBALIMBALI KATIKA KILELE CHA MAADHIMISHO YA SIKU YA UKIMWI DUNIANI-DESEMBA 1, 2017

 Wananchi mbalimbali wakiwa kwenye maandamano wakati wa kilele cha maadhimisho ya siku ya Ukimwi duniani Desemba 1, 2017 yaliofanyika katika viwanja vya mnazi mmoja jijini Dar es Salaam mgeni rasmi wa maadhimisho hayo ni Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Samia Suluhu Hassan.
(PICHA ZOTE NA PHILEMON SOLOMON)
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Samia Suluhu Hassan pamoja na viongozi wengine wa serikali wakipokea maandamo (hayapo pichani) wakati wa kilele cha maadhimisho ya siku ya Ukimwi duniani Desemba 1, 2017 yaliofanyika katika viwanja vya mnazi mmoja jijini Dar es Salaam
 Wananchi wakiwa  kilele cha maadhimisho ya siku ya Ukimwi duniani Desemba 1, 2017 yaliofanyika katika viwanja vya mnazi mmoja jijini Dar es Salaam
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Mkurugenzi wa Uragibishi na Habari kutoka Tume ya Kudhibiti UKIMWI Tanzania(TACAIDS), Jumanne Issango.
 Wanachi wakipima shinizo la Damu wakati wa maadhimisho hayo.
 Mratibu kutoka Shirika lisilo la kiserikali Voice of African Mothers Tanzania (VAM-TZ), Bi Mary Makinda akimuelezea  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Samia Suluhu Hassan huduma wanazotoa za mapambano ya Ukimwi alipotembelea mabanda katika kilele cha maadhimisho ya siku ya Ukimwi duniani Desemba 1, 2017 yaliofanyika katika viwanja vya mnazi mmoja jijini Dar es Salaam.
 Mkurugenzi wa Sera na Utafiti wa Tume ya Kudhibiti UKIMWI Tanzania(TACAIDS), Richardi Ngirwa akimuelezea Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Samia Suluhu Hassan kuhusiana elimu wanazotoa kwa wanachi  dhidi ya maambukizi Ukimwi.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Samia Suluhu Hassan pamoja na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama wakiwa kwenye picha ya pamoja na watumishi wa Tume ya Kudhibiti UKIMWI Tanzania (TACAIDS) alipotembelea banda hilo wakati wa kilele cha maadhimisho ya siku ya Ukimwi duniani Desemba 1, 2017 yaliofanyika katika viwanja vya mnazi mmoja jijini Dar es Salaam.
Msanii wa nyimbo za uswahilini, Seleman Jabir ‘Msaga Sumu  akitoa burudani katika maadhimisho hayo.

No comments :

Post a Comment