Na Said Mwishehe, Blogu ya Jamii.
TASNIA ya habari imeombwa kuendeleza mapenzi baina yao kama walivyoonesha katika ugonjwa wa Mayage S. Mayage aliyefariki juzi.
Hayo
yamesemwa leo mchana huu na Padre John kaniki wa Kanisa Katoliki
katika ibada ya mazishi ya marehemu Mayage iliyofanyika nyumbani kwake
Mbweni jijini Dar es Salaam.Padre Kaniki amesema maumivu aliyokua
akipata kitandani Mayage wakati anaumwa aliyatoa kwa ajili ya watu
anaowapenda ikiwemo wanahabari wenzie.
Alisema
msiba ni sehemu ya kutubia kwa wale wanaobaki hivyo ni vema wote kuwa
wanyenyekevu kwa Mungu.Amesema yeye binafsi alimfahamu Mayage S. Mayage
katika kipindi ambacho alikuwa anaunwa kwani alikuwa akimfanyia maombi
na alichojifunza ni upendo na uvumilivu.
"Alikuwa
ni mtu mwenye upendo na huruma, ni vema tukaendeleza mema yake na kubwa
zaidi ni kumuombea kwa Mungu, "amesema Padre Kaniki.
Mayage
S. Mayage wakati wa uhai wake amesoma katika vyuo mbalimbali vya ndani
na nje na baada ya kuhitimu amefanya kazi katika maeneo mbalimbali.
Ilipofika
mwaka 1995 ndipo alipojiunga na kampuni ya magazeti ya Habari
Coparation ambayo sasa ni New Habari na baadae alikwenda gazeti la Raia
Tanzania.
Akizungumza
katika maziko ya Mayage S. Mayage, Mhariri Mtendaji wa New Habari,
Absaloum Kibanda amemuelezea Mayage kama mwandishi aliyeacha alama ya
ujasiri na uthubutu katika taaluma. Kibanda amesema mchango wa Mayage
katika tasnia ya habari na hasa uchambuzi wa habari za siasa."Mimi na
Mayage pamoja na wengine tuliojaaliwa pamoja Habari Coparation,
anayeweza kumzungumzia vizuri Mayage ni mhariri na mwalimu wetu
kitaalum.
Safari
ya Mwisho ya aliyekuwa Mwandishi Mkongwe hapa nchini,Marehemu Mayage
Steven Mayage imefanyika jioni ya leo katika makaburi ya Mbweni
Maputo,Kinondoni jijini Dar Es Salaamu
Wawakilishi
kutoka Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,Ikulu John Chacha na Ankal Issa
Michuzi kwa pamoja wakiweka shada la Maua juu ya kaburi la marehemu
mara baada ya kufanyika maziko yake jioni ya leo katika makaburi ya
Mbweni Maputo,Kinondoni jijini Dar Es Salaam.
Mbunge
wa Jimbo la Mtama,Mh Nape Nnauye akiweka shada la Maua juu ya kaburi la
marehemu mara baada ya kufanyika maziko yake jioni ya leo katika
makaburi ya Mbweni Maputo,Kinondoni jijini Dar Es Salaam.
Mmoja
wa aliyefanya kazi na Marehemu Mayage,Ndugu Haji Dillunga akiweka shada
la Maua juu ya kaburi la marehemu mara baada ya kufanyika maziko yake
jioni ya leo katika makaburi ya Mbweni Maputo,Kinondoni jijini Dar Es
Salaam.
Sala
ya Maziko ya Marehemu Mayage Steven Mayage ikiendelea katika Makaburi
ya Mbweni Maputo,kabla ya kumlaza mpendwa wetu katika nyumba yake ya
Milele,jioni
No comments :
Post a Comment