Saturday, December 9, 2017

MAADHIMISHO YA MIAKA 56 YA UHURU YALETA NEEMA KWA FAMILIA YA BABU SEYA, NI BAADA YA RAIS MAGUFULI KUTOA MSAMAHA KWA WAFUNGWA


1
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiingia kwa gari maalum akiwa na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Venance Mabeyo wakati wa maadhimisho ya miaka 56 ya Uhuru wa Tanzania yaliyofanyika kwenye uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma ambako ndiyo makao makuu ya Nchi. maadhimisho hayo yamehudhuriwa na viongozi mbalimbali wa serikali ,Mabalozi wa wanaoziwakilisha nchi zao hapa nchini, viongozi wa vyama vya siasa, Viongozi wa dini pamoja na wananchi wa viunga vya mji wa Dodoma, Mh. Rais Dkt. John Pombe Magufuli pia amemsamehe Nguza Viking “Babu Seya” na Mwanaye  Johnson Nguza “Papii Kocha” waliokuwa wamefungwa Kifungo cha Maisha Gerezani.(PICHA NA JOHN BUKUKU-FULLSHANGWE-DODOMA)
2  4
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akikagua gwaride huku akiongozwa  na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Venance Mabeyo wakati wa maadhimisho ya miaka 56 ya Uhuru wa Tanzania yaliyofanyika kwenye uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma
5 6 7
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akielekea jukwaa kuu mara baada ya kukagua gwaride huku akiongozwa  na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Venance Mabeyo wakati wa maadhimisho ya miaka 56 ya Uhuru wa Tanzania yaliyofanyika kwenye uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma
8
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Mh.Jenista Mhagama Waziri Waziri wa Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu baada ya kukagua gwaride katika maadhimisho ya miaka 56 ya Uhuru wa Tanzania yaliyofanyika kwenye uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma
9
Picha mbalimbali zikionyesha Vikosi vya Ulinzi vikitoa heshima kwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli Amiri jeshi mkuu wa majeshi ya Uinzi wakati wa maadhimisho ya miaka 56 ya uhuru kwenye uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma leo.
3
10 11 12 13 14
Kikosi cha Makomandoo wa Jeshi la Ulinzi JWTZ kikipita kwa Gwaride la heshima mbele ya Rais Dkt. John Pombe Magufuli.
15 16
Baadhi ya wananchi mbalimbali waliohudhuria katika maadhimisho hayo wakiwa jukwaa kuu.
18
Makomandoo wakionyesha onyesho lao la kuokoa kiongozi aliyetekwa kwa kushuka na Helkopta ya kijeshi.
20
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akihutubia wakati wa maadhimisho hayo yaliyofanyika kwenye uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma.

No comments :

Post a Comment