CHAMA Cha Maofisa Uhusiano wa Umma
(PRST) kimezinduliwa jijini Dar es Salaam, ambapo maudhui makubwa ya
kuundwa kwa umoja huo ni kutambulika rasmi kama taasisi na kupanuana
mawazo ya utumishi miongoni mwa wanachama, ikiwa ni pamaoja na kuendesha
shughuli zao kwa utaratibu maalum.
Akihutubia katika uzinduzi huo,
mgeni rasmi ambaye ni Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na
Michezo, Ndege Makula aliwasisitizia wanachama juu ya kudumisha maadili
ya umma katika utumishi wao huku akitilia mkazo suala la kujali misingi
ya taaluma na matakwa ya sheria katika kulitumikia taifa.
“Nawaomba mtambue kuwa kupitia
ummoja wenu huu ninyi mmebeba dhamana kubwa ya kuhakikisha mnatumika
ipasavyo kwa wananchi, kwa hiyo cha muhimu ni kuzingatia maadili na
misingi ya taaluma yenu ikiwa ni pamoja na kufuata sheria inataka nini,
vinginevyo niwatakieni utumishi mwema katika nafasi hizi muhimu kwa
jamii,” alisema Makula.
No comments :
Post a Comment