Mkurugenzi wa Mawasiliano Airtel Tanzania Beatrice Singano – kulia akiongea jana wakati wa uzinduzi wa bando za ‘SMATIKA na Yatosha Intaneti’ mpya ambapo mteja wa Airtel itamuwezesha mteja wa Airtel KUSMATIKA NA GB 1 ya Yatosha Intaneti kwa siku tatu mfululizo kwa shilingi elfu mbili. Kushoto ni Mkurugenzi wa Masoko Airtel Tanzania Isack Nchunda.
Mkurugenzi wa Mkurugenzi wa Masoko Airtel Tanzania Isack Nchunda – kushoto akiongea jana wakati wa uzinduzi wa bando za ‘SMATIKA na Yatosha Intaneti’ mpya ambapo mteja wa Airtel itamuwezesha mteja wa Airtel KUSMATIKA NA 1GB ya Yatosha Intaneti kwa siku tatu mfululizo kwa shilingi elfu mbili. Kushoto ni Mawasiliano Airtel Tanzania Beatrice Singano.
Mkurugenzi wa Masoko Airtel
Tanzania Isack Nchunda na Mawasiliano Airtel Tanzania Beatrice Singano
wakionyesha bango baada ya kuzindua bando za ‘SMATIKA na Yatosha Intaneti’ mpya ambapo mteja wa Airtel itamuwezesha mteja wa Airtel KUSMATIKA NA 1GB ya Yatosha Intaneti kwa siku tatu mfululizo kwa shilingi elfu mbili.
……………
- ‘SMATIKA NA 1GB Yatosha Intaneti inayokupa muda mrefu kwa gharama nafuu zaidi.
Airtel Tananzania Mtandao bora kwa
Smartphone yako imewapatia wateja wake uhuru zaidi kwa kuwaletea bando
mpya za ‘SMATIKA na Yatosha Intaneti’ maalum kwa watumiaji wa huduma za
intaneti.
Mkurugenzi wa Masoko wa Airtel
Isack Nchuna wakati wa hafla ya kuzindua ‘SMATIKA na Yatosha Intaneti,
alisema “Airtel itaendelea kuleta huduma zenye ubora na ubunifu wa hali
ya juu ili kuendelea kuwa sambamba na mahitaji ya wateja katika huduma
za intaneti ambapo kwa zaidi ya mwaka mmoja sasa Airtel imejiwekea
mikakati endelevu mingi ili kukidhi uhitajika na wateja wote”
“Tuaendelea kudhihirisha dhamira
yetu ya kutoa suluhisho la mawasiliano
kupitia uzinduzi wa ‘SMATIKA na
Yatosha Intaneti’ kwa kutoa huduma nafuu ya Intaneti kwa watumiaji wote
nchini huku tukiweka kipaumbele zaidi katika ubora wa mtandao pamoja na
kuwapatia wateja uhuru zaidi” aliongeza Nchunda
“SMATIKA na Yatosha Intaneti’ ni
zawadi ya awali kabisa tunayowapatia watumiaji wa Airtel katika msimu
huu wa sikukuu, tunaamini kuwa ndani ya msimu huu wa sikukuu wateja
wanauhitaji mkubwa sana wa intaneti katika kukamilisha shamrasharna
wakiwa wanawasiliana na ndugu, jamaa na marafiki wakati wote!”
Akifafanua zaidi Mkurugenzi wa
Mawasiliano wa Airtel Tanzania Bi Beatrice Singano alisema Bando za
‘SMATIKA na Yatosha Intaneti’ zinatoa uhuru kwa wateja wote wa airtel
kujichagulia bando la intaneti KABAMBE wakati wowote.
“Mteja wa Airtel ataweza kunufaika
na SMATIKA na Yatosha Intaneti kwa gharama nafuu ya hadi shilingi 200
na kujipatia MB 40, vilevlie mteja ataweza KUSMATIKA NA 1GB ya Yatosha Intaneti kwa siku tatu mfululizo kwa shilingi elfu mbili tu” alieleza Bi Singano
“kujiunga na ‘SMATIKA na Yatosha Intaneti’ unatakiwa kupiga *149*99# kisha chagua 5 Yatosha Intanet vilevile unaweza kujiunga kupitia Airtel Money kwa kupiga *150*60# kisha chagua Yatosha Intanet”.
Airtel Tanzania imekuwa katika
programu ya uboreshaji wa miundombinu ya mawasiliano yake ili
kukamilisha lengo lake la kutoa mawasiliano bora na yenye uhakika kwa
kutumia teknolojia ya kisasa ya U900. Tayari Airtel imezindua maboresho
ya mtandao wake kwa kutumia teknolojia hiyo ya U-900 kwenye mikoa ya
Arusha, Dar es salaam, Dodoma, Morogoro na Mwanza huku ikiendelea
kuwahakikishia wateja wake mawasiliano bora hasa katika maeneo ya nje na
ndani ya majengo marefu au yenye uhitaji zaidi.
No comments :
Post a Comment