Waziri wa Nishati, Dkt. Medard
Kalemani (katikati mbele) na Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo
(kushoto mbele) wakiendelea na ziara katika kampuni ya kutengeneza
transfoma za umeme ya TANELEC, iliyopo jijini Arusha. Kulia mbele ni
Meneja Mkuu wa kampuni hiyo, Zahir Saleh
Waziri wa Nishati, Dkt. Medard
Kalemani akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili kwenye ofisi
za kampuni ya kutengeneza transfoma za umeme ya TANELEC zilizopo jijini
Arusha.
Mmoja wa mafundi wa kampuni ya kutengeneza transfoma za umeme ya TANELEC akipiga rangi transfoma mojawapo
Meneja Mkuu wa kampuni ya
kutengeneza transfoma za umeme ya TANELEC, Zahir Saleh (kulia)
akimwonesha Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani moja ya mifuniko ya
transfoma za umeme inayotengenezwa na kampuni hiyo.
Msimamizi wa Idara ya Vyuma,
Zakayo Mmbaga (kulia) akionesha jinsi mashine ya kukunja vyuma
inavyofanya kazi kwa Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani (wa pili
kushoto)
Meneja Mkuu wa kampuni ya
kutengeneza transfoma za umeme ya TANELEC, Zahir Saleh (kulia) akielezea
mafanikio ya kampuni hiyo kwa Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani
(wa pili kulia mbele). Kushoto mbele ni Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho
Gambo
Mafundi wa kampuni ya kutengeneza transfoma za umeme ya TANELEC, wakiendelea na kazi
Meneja Mkuu wa kampuni ya
kutengeneza transfoma za umeme ya TANELEC, Zahir Saleh (kushoto mbele)
akielezea matumizi ya mashine ya kukata bati kwa Waziri wa Nishati, Dkt.
Medard Kalemani (kulia)
Waziri wa Nishati, Dkt. Medard
Kalemani (katikati) akitoa maelekezo kwa watendaji na wafanyakazi wa
kampuni ya kutengeneza transfoma za umeme ya TANELEC.
Meneja Mkuu wa kampuni ya
kutengeneza transfoma za umeme ya TANELEC, Zahir Saleh (kulia) akielezea
usukaji wa nyaya za transfoma za umeme unavyofanyika katika kiwanda
hicho.
Waziri wa Nishati, Dkt. Medard
Kalemani (katikati) akipanda mti kama kumbukumbu ya ziara yake katika
kampuni ya kutengeneza transfoma za umeme ya TANELEC, iliyopo jijini
Arusha.
Waziri wa Nishati, Dkt. Medard
Kalemani ( wa nne kutoka kulia waliokaa mbele) na Mkuu wa Mkoa wa
Arusha, Mrisho Gambo ( wa tatu kutoka kulia waliokaa mbele) wakiwa
katika picha ya pamoja na watendaji wa kampuni ya kutengeneza transfoma
za umeme ya TANELEC, Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) na Wakala wa
Nishati Vijijini (REA) mara baada ya kumalizika kwa ziara hiyo.
………………..
Na Greyson Mwase, Arusha
Novemba 22, 2017
Waziri wa Nishati, Dkt. Medard
Kalemani tarehe 22 Novemba, 2017 alifanya ziara katika kampuni ya
kuzalisha transfoma za umeme ya TANELEC iliyopo jijini Arusha lengo
likiwa ni kukagua shughuli za kampuni hiyo pamoja na kuangalia...
namna ya
kutatua changamoto katika uzalishaji wa vifaa vya umeme nchini.
Akiwa ameambatana na Mkuu wa Mkoa
wa Arusha, Mrisho Gambo pamoja na watendaji kutoka Wizara ya Nishati,
Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) na Wakala wa Nishati Vijijini (REA),
Dkt. Kalemani alisema mara baada ya kukagua shughuli za kampuni hiyo na
kujiridhisha uwezo wa kampuni hiyo katika uzalishaji wa transfoma, ni
wakati wa TANESCO na REA kujipanga upya katika mahitaji ya transfoma za
kutosha na kuwasilisha mahitaji hayo kwa kampuni husika na kuongeza kasi
ya miradi ya umeme nchini.
Alifafanua kuwa mapema Juni mwaka
huu Serikali kupitia Wizara ya Nishati ilipiga marufuku uingizwaji wa
nguzo za zege na transfoma ili kuepuka gharama kubwa na tatizo la
kuchelewa kwa miradi.
Aliendelea kusema kuwa baada ya
kutoa agizo hilo, ameamua kufanya ziara ili kubaini uwezo na mahitaji
halisi ya transfoma za umeme ambapo amebaini kuwa kampuni hiyo ina
uwezo wa kuzalisha transfoma za umeme 10,000 wakati mahitaji halisi ya
transfoma za umeme nchini yakiwa ni 6,500
Alisema kutokana na uwezo mkubwa
wa uzalishaji wa transfoma katika kampuni hiyo, ni wakati wa TANESCO na
REA kukaa pamoja na kuainisha upya mahitaji ya transfoma za umeme
nyingi zaidi ili kuendana na kasi ya utekelezaji wa miradi ya umeme
nchini.
Dkt. Kalemani mbali na TANESCO na
REA, aliwataka wakandarasi wanaotekeleza miradi ya REA Awamu ya Tatu
kuanza kuainisha mahitaji yao mapema kwa kampuni hiyo ili pasiwepo na
kikwazo cha utekelezaji wa miradi ya umeme vijijini.
“ Nimeambiwa kuwa wakandarasi
wachache wameagiza transfoma za umeme katika kampuni ya TANELEC, nitoe
fursa hii kuwataka wakandarasi wote nchini kuagiza transfoma za umeme
mara moja na kuanza utekelezaji wa miradi yao kwa kasi kubwa, pasiwepo
na kisingizio cha kukosekana kwa transfoma za umeme,”alifafanua Dkt.
Kalemani
Katika hatua nyingine Waziri
Kalemani aliitaka kampuni ya TANELEC kuanza kulipa gawio lake kwa
serikali kupitia Msajili wa Hazina kuanzia mwaka huu.
Alisema Serikali inamiliki
asilimia 30 ambapo asilimia 20 zinamilikiwa na TANESCO na asilimia 10
kupitia Shirika la Maendeleo Nchini (NDC)
Naye Meneja Mkuu wa Kampuni ya
TANELEC, Zahir Saleh akielezea biashara ya transfoma za umeme katika
kampuni hiyo alisema kampuni hiyo imefanikiwa kwa kiasi kikubwa
kusambaza transfoma katika nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki kama
vile Tanzania, Kenya na Uganda na nchi nyingine kama vile, Nigeria,
Zimbabwe na Ethiopia.
Alifafanua kuwa, wateja wakubwa wa
transfoma hizo ni pamoja na wazalishaji wa umeme, wakandarasi wa
miradi ya umeme na wateja binafsi na kuongeza kuwa kampuni hiyo
imejipanga zaidi kuhakikisha inaongeza kasi ya uzalishaji ili
kukabiliana na mahitaji ya transfoma za umeme mara baada ya serikali
kupiga marufuku uingizwaji wa transfoma za umeme kutoka nje ya nchi.
Alisema kuwa kampuni imepanga
kuongeza ajira kutoka wafanyakazi 120 hadi 150 ili kuongeza kasi ya
uzalishaji na usambazaji wa transfoma ndani na nje ya nchi.
No comments :
Post a Comment