Mgeni rasmi katika Mahafali ya
Chuo cha Maendeleo ya Jamii Tengeru ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya
Arusha Bw. Gabriel Fabiani akikabidhi zawadi kwa mwanafunzi bora wa
shahada ya kwanza Maendeleo ya Jamii Usimamizi wa program za maendeleo
ya jaimii Bi.Fotunata Kaniki.
Wajumbe wa bodi ya Chuo cha
Maendeleo ya Jamii Tengeru wakiwa katika picha ya pamoja na badhi ya
wahitimu leo Tengeru Jijini Arusha.
Kaimu Mkuu wa Chuo cha Maendeleo
ya Jamii Tengeru Dr. George Bakari akiwahutubia wahitimu mbalimbali wa
Chuo hicho leo Tengeru jijini Arusha .
Mgeni rasmi katika Mahafali ya
Chuo cha Maendeleo ya Jamii Tengeru ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya
Arusha Bw. Gabriel Fabiani akitoa hotuba yake kwa wahitimu mbalimbli
hawapo pichani leo katika chuo hicho Tengeru nje kidogo ya jiji la
Arusha.
Mgeni rasmi katika Mahafali ya
Chuo cha Maendeleo ya Jamii Tengeru ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya
Arusha Bw. Gabriel Fabiani akitoa hotuba yake kwa wahitimu mbalimbli
hawapo pichani leo katika chuo hicho Tengeru nje kidogo ya jiji la
Arusha.
………..
Mgeni rasmi katika Mahafali ya
Taasisi ya Maendeleo ya Jamii Tengeru amewataka wahitimu mbalimbali
Katika chuo hicho kutafsiri elimu waliyoipata kwa vitendo akiwataka
kutanguliza maslahi ya Jamii badala ya maslahi binafsi ambayo
...
yamelitafuna Taifa kwa kipindi kirefu sasa.
Aidha mgeni rasmi hiyo bwana
Gabriel Fabian ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Arusha amesema wasomi
wamelitia Taifa hasara kwa kusaini mikataba mibovu na kupokea rushwa
akiwataka wahitimu hao kutumia elimu kwa manufaa ya wale walioikosa na
Taifa kwa ujumla.
Aidha amewataka wahitimu hao
kuangalia fursa nyingine nje ya taaluma yao na kuacha tabia yakutaka
ajila za mfumo rasmi ambazo zina ushindani mkubwa kwa kuwa taaluma Kama
ya kwao inatolewa na taasisi nyingine za elimu ya Juu .
Mkuu huyo wa Wilaya pia
amesisitiza matumizi sahihi ya Maktaba akisema kuwa waihitimu wengi siku
hizi wanatumia makaburasha na vitini vya wahitimu wa zamani badala ya
kusoma vitabu ambavyo uandikwa na wanazuoni wakubwa duniani.
Wakati huohuo Makamu Mkuu wa Taasisi ya Chuo cha Maendeleo ya Jamii Tengeru Dk.George Bakari amesema
Kwasasa chuo chake kipo katika
mageuzi makubwa ya kuhakikisha chuo hicho kinakua kitaaluma kwa kujenga
mahusiano makubwa na taasisi nyingine za kitaaluma ndani na nje ya nchi
ikiwemo kubadilishana wahadhili na kujenga uwezo wa kitafiti .
Dr. Bakari ameongeza kuwa Chuo
chake kwa sasa kinaendelea pia kuchukua hatua anwai za kuendeleza
watumishi wanataaluma na wasio wanataaluma kielimu ili waweze
kujiimarisha kielimu ili kuendana na mabadiliko yaliyopo sasa katika
wigo mpana wa sayansi na teknolojia.
Chuo hiki chini ya Mwanazuoni huyo
pia kinaratibu uanzishwaji wa bodi ya taaluma ya kada ya maendeleo ya
Jamii hapa nchini ambapo ametumia fursa hiyo ya Mahafali kuwataka
wahitimu kujiunga mara moja na umoja wa wanataaluma wa maendeleo ya
Jamii.
Taasisi ya Maendeleo ya Jamii
Tengeru imewatunuku wahitimu wake astashahada,shahada,na stashahada ya
kwanza ya maendeleo ya Jamii mwaka wa masomo 2016/17
No comments :
Post a Comment