Na Waandishi Wetu, Mwanza na Dar..
*Subash Patel asema Rais ameweka rekodi ya kihistoria
*Azindua viwanda vya juisi, dawa vitakavyoajiri mamia ya watu
ZIARA
ya Rais John Pombe Magufuli jijini Mwanza imepokewa kwa furaha na
wananchi wa mikoa ya Kanda ya Ziwa ambapo ikiwa ni ...
miaka miwili sasa
tangu aingie madarakani, uzinduzi wa viwanda na miradi mingine ya
maendeleo ni ishara ya kazi kubwa iliyofanywa na Serikali yake.
Mwanzilishi
na Mkurugenzi Mkuu wa Motisun Group Limited, inayomiliki viwanda
mbalimbali hapa nchini kikiwemo cha jusi aina ya Sayona, Bw. Subash
Patel, akiwakilisha maoni ya wawekezaji wengine walioguswa pia na
utendaji wa Rais Magufuli amemweleza Rais kuwa kiongozi aliyeweka
historia katika kutekeleza uanzishwaji wa viwanda nchini vingi vikiwa
ndani ya kipindi kifupi.
Akizungumza
katika mkutano wa hadhara jana Jijini Mwanza, Bw. Patel amesema kuwa
historia inaonesha Rais Magufuli ni Rais pekee ndani ya miaka miwili
aliyeweza kuzindua viwanda vingi zaidi na kuruhusu mataifa mbalimbali
kuwekeza nchini.
“Kwa
umri huu nilionao nimebahatika kufanya kazi na Marais wa Awamu zote
ikiwa wewe mmoja wapo. Tangu uhuru, wewe umekuwa wa kipekee uliyetambua
umuhimu wa viwanda na maslahi ya wananchi kutokana na faida ya viwanda
hivyo,” alisema Bw. Patel.
Aidha,
Bw. Patel ameahidi kuunga mkono juhudi za Rais Dkt Magufuli za
kuipeleka Tanzania katika uchumi wa kati kupitia wiwanda. Ameongeza kuwa
kazi kubwa ya kampuni hiyo ni kuungana na Rais katika azma yake.
Ameongeza
kuwa ifikapo mwezi Juni mwaka 2018 kampuni hiyo inatarajia kuzindua
viwanda vingine vitano vitakavyozalisha bidhaa mbalimbali ikiwemo
matunda, rangi za nyumba vinywaji na chuma.
Kiwanda
cha vinywaji baridi cha Sayona jijini Mwanza kimejengwa kwa muda wa
mwaka mmoja na nusu na kina uwezo wa kuzalisha chupa 1,200 kwa dakika
moja. Tayari kiwanda hicho kimezalisha ajira za watu 200 na kinaungana
na kiwanda kingine cha vinywaji baridi cha Sayona kilichopo Mboga Mkoani
Pwani kusindika matunda ya wakulima na kuinua hali zao za maisha.
“Uzinduzi
wa viwanda hivi ni ishara ya wazi kuwa sera za Serikali yetu ni sahihi
na zinalenga kuwasaidia wananchi kupata ajira lakini na bidhaa za
uhakika. Naomba watu wajue hakuna hela utaipata katika Serikali hii bure
tu. Watu wawekeze kwenye viwanda kwani hata hawa wafanyabiashara
wasingewekeza wasingepata hela ya Serikali.
“Sasa
wale wapiga dili na mafisadi wajue wataishia jela tu hakuna fedha ya
Serikali itakayoliwa kirahisi katika zama hizi. Serikali itafanyakazi na
wawekezaji wote walioamua kuunga mkono sera yetu ya viwanda na
tutaendelea kutatua changamoto zinazowakabili,” alisema Rais.
Ndoto
na dhana nzima ya Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais Dkt.
Magufuli ni Ujenzi wa Viwanda nchini ambapo mpaka sasa viwanda takribani
3306 vimefungulia ndani ya miaka miwili ya uongozi wa Serikali ya Awamu
ya Tano.
Akiwa
ziara Mwanza ambako pia amezindua kiwanda cha dawa za binadamu, daraja
la waenda kwa miguu la Furahisha na viwanda vingine kadhaa, Rais
Magufuli ameendelea kusisitiza juu ya ajenda yake ya kuleta mageuzi
nchini.s.
No comments :
Post a Comment