Askofu wa Kanisa la Good News For
All Ministry Dkt. Charles Gadi (katikati) akizungumza na waandishi wa
habari (hawapo pichani) kuhusu maombi maalum ya kuzuia mvua zisilete
madhara kwa jamii mapema hii leo jijini Dar es Salaam, kushoto ni
Mchungaji James Mwageni na kulia ni Mchungaji Palemo Massawe.
Askofu wa Kanisa la Good News For
All Ministry Dkt. Charles Gadi (katikati) akifanya maombi maalum ya
kuzuia mvua zisilete madhara kwa jamii mapema hii leo jijini Dar es
Salaam, kushoto ni Mchungaji James Mwageni na kulia ni Mchungaji Palemo
Massawe.
……………..
Na: Frank Shija – MAELEZO
Rais
John Pombe Magufuli amezidi kupongezwa kwa namna ambavyo amekuwa mstari
wa mbele katika kusimamia rasilimali za Taifa ili ziweze kuwanufaisha
wananchi wote.
Pongezi hizo zimetolewa leo Jijini Dar es Salaam na Mwenyekiti wa Good News for All Ministry,
Askofu Charles Gadi alipokuwa...
akizungumza na Waandishi wa Habari pamoja
na kufanya maombi ya kuzuia kunyesha kwa mvua zenye madhara.
“Napenda
kuchukua nafasi hii kwa dhati kabisa kama kiongozi wa dini kumpongeza
Rais Magufuli kwa kufanikiwa kusimamia kikamilifu rasilimali za nchi
yetu hususan eneo la madini ya dhahabu na vito,hadi kuwezesha kurejeshwa
sehemu ya malimbikizo ya kodi ambayo huenda tusingeipata kama siyo
jitihada zake”, alisema Askofu Gadi.
Askofu
Gadi amesema kuwa kama si ujasiri aliouonyesha Rais Magufuli katika
kupigania raslimali za nchi, kama isingekuwa msimamo wake wa
kutoyumbishwa na makampuni ya madini huenda makubaliano yasingefikiwa
kama ilivyo sasa.
Awali
akizungumza kabla ya kuanza kuomba kuhusu kuzuia mvua zenye madhara
kunyesha kwa lengo la kuokoa maisha ya watanzania wanyonge jambo
linaloelezwa kuwa ni hatua nzuri kwa Serikali kuweka misingi yenye
mikubwa na imara.
Askofu
Gadi amesema kuwa wamekuwa na desturi ya kufanya maombi mbalimbali ya
kuliombea Taifa kuepukana na majanga mbalimbali yakiwemo mafuriko, hivyo
maombi haya maalum ya kuzuia mvua yamekuja wakati muafaka ambapo
Mamlaka ya Hali ya Hewa wametoa tahadhari kuhusu uwepo wa mvua kubwa.
Aidha,
Kiongozi huyo wa Kiroho amesema kuwa wameleta maombi hayo maalum ya
kuzuia mvua zenye madhara kwa imani kwamba mvua za Mungu hazileti
madhara mabaya kwa watu, kwani alishaapa baada ya gharika ya Nuhu kwamba
hatakaa aiangamize dunia tena kwa maji.
No comments :
Post a Comment