Thursday, November 9, 2017

UMOJA WA VIJANA WALIOSOMA NCHINI CHINA (CAAT) WATEMBELEA HIFADHI YA SELOUS KATIKA KUUTANGAZA UTALII WA NDANI KWA NJIA YA RELI YA TAZARA

Umoja wa Vijana waliosoma nchini China (CAAT) wametembelea katika hifadhi ya ya Taifa ya Selous ili kutangaza utalii wa ndani kwa njia ya treni ya TAZARA. Akizungumza mwenyekiti wa umoja huo, Dkt. Liggyla Vumilia alisema kuwa wameamua kuandaa kampeni ya kutangaza utalii wa ndani kwa njia ya treni ya TAZARA hasa wa mikoa ya kusini mwa Tanzania ambao umekuwa ukisahaulika. 

Kampeni hiyo imeandaliwa na Umoja wa Vijana waliosoma nchini China (China Alumni Association of Tanzania -CAAT) kwa kushirikiana na Bodi ya Utalii Tanzania - (TTB) na TAZARA. PICHA ZOTE NA KAJUNASON/MMG - SELOUS-MATAMBWE, MOROGORO.
Umoja wa Vijana waliosoma nchini China (CAAT) wakifurahia ndani ya treni ya TAZARA wakati wakielekea ndani ya hifadhi ya Selous.
                                                                                           Ilikuwa ni furaha kila kona.
SOMA ZAIDI »

No comments :

Post a Comment