Waziri
wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Ummy Mwalimu akisaini
kitabu cha wageni mara baada ya kufika kwenye hospitali ya Magonjwa ya
kuambukiza Kibong’oto Mkoani Kilimanjaro,kushoto ni Mkuu wa Mkoa huo
Mhe.Anna Mghirwa
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro
Mhe.Anna mghirwa akiongea wakati wa ufunguzi wa kiyuo hicho ambacho
kitakuwa kikihudumia wachimbaji wa madini na familia zao kutokana na
kifua kikuu na kudhurika na magonjwa ya mfumo wa hewa
Baadhi ya wachimbaji wa madini kutoka Mererani ambao walishiriki ufunguzi wa kituo hicho
Baadhi
ya watumishi wa Hospitali ya Kibong’oto wakimsikiliza Waziri Ummy
Mwalimu(hayupo pichani)wakati akihutubi ambapo alisema kituo hicho ni
miongoni mwa vituo 11 vilivyojengwa katika nchi 10 za SADC
Waziri wa Afya pamoja na viongozi wa Mkoa,Mbunge pamoja na wadau wa madini wakikata utepe kuashiria ufunguzi wa kituo hicho
Waziri
Ummy Mwalimu(wa kwanza kushoto),Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Mhe.Anna
Mghirwa(kulia) walikagua chumba chenye mashine ya Uchunguzi (Xray)
iliyofungwa kwenye kituo hicho
……………
Na.Catherine Sungura,WAMJW,Siha
Shughuli
za uchimbaji madini duniani kote zinatambulika kama ni shughuli
hatarishi kwa afya ya binadamu kutokana na urahisi wa kudhurika pia
athari kwenye afya ya mapafu kutokana na vumbi zito
Hayo
yamesemwa jana na Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na
Watoto Ummy Mwalimu wakati wa ufunguzi wa kituo cha kisasa cha... kutoa
huduma za Kifua Kikuu,Ukimwia na Magonwa yatokanayo na shughuli za
uchimbaji madini katika hospitali ya magonjwa ya kuambukiza Kibong’oto
iliyopo Mkoani Kilimanjaro
Waziri Ummy amesema shughuli za
uchimbaji humuweka mchimbaji kwenye hatari zaidi ya kupata kwa urahisi
ugonjwa wa Kifua Kikuu na Magonjwa mengine sugu ya mfumo wa njia ya
hewa,vile vile shughuli za kijamii,kiuchumi na kiutamaduni katika maeneo
ya migodi zimekua zikichochea kasi ya maambukizi ya Ukimwi katika
maeneo hayo.
“Kutokana na changamoto hizi na
ili tupunguze tatizo LA Kifua Kikuu na UKIMWI katika sekta ya
madini,mwaka 2015 nchi kumi za SADC kwa pamoja ziliomba fedha katika
mfuko wa Dunia wa Kudhibiti magonjwa ya UKIMWI,Kifua Kikuu na
Malaria(Global fund ATM) ili kukabiliana na tatizo hili katika sekta ya
madini”(TB in the Mining Sector(TIMS)
Aidha,alisema tangu kuanza
kutekelezwa kwa mradi huo Januari,2016,tayari matokeo ya utafiti
zilizofanyika maeneo ya migodi yameonesha kuwepo kwa kiwango kidogo cha
ufahamu na uelewa wa masuala ya Kifua Kikuu,UKIMWI na magonjwa
yatokanayo na shughuli za uchimbaji miongoni kwa wachimbaji na jamii
inayowazunguka.
” wachimbaji wadogo wadogo
wameendelea kuathirikanna vumbi LA silika kutokana na kutumia dhana duni
za uchimbaji usiozingatia masharti ya udhibiti wa vumbi,licha ya sekta
hii kuchangia kwa kiasi kikubwa pato LA Taifa,hali a upatikanaji wa
huduma za afya kwenye migodi si ya kuridhisha”
Kituo
hicho cha kisasa ambacho ni cha kwanza nchini kitakua mfano na
kitasaidia kuokoa maisha na ulemavu utokanao na shughuli za uchimbaji
kutokana sehemu zingine nchini,kimefungwa vifaa vya uchunguzi ikiwepo
xray na kupatiwa daktari bingwa na wataalamu wa maabara na mionzi

No comments :
Post a Comment