Tuesday, November 21, 2017

TAASISI YA KIFEDHA YATENGA DAU LA PAUNDI MILIONI 300 KUINUNUA NEWCASTLE UNITED

Taasisi ya Kifedha inayoongozwa na mfanyabiashara mwanamke Muingereza Amanda Staveley imewasilisha dau la paundi milioni 300 kuinunua klabu ya Newcastle United.

Kampuni hiyo ya PCP Capital Partners imefanya mazungumzo na mmiliki wa klabu hiyo Mike Ashley kwa mwezi sasa, na taarifa sasa zinasema dau hilo limetengwa.

Uongozi wa klabu ya Newcastle haujazungumzia lolote kuhusiana na ofa hiyo, ingawa chanzo kimoja ndani ya klabu hiyo hakijaridhika na kiasi cha dau hilo.

No comments :

Post a Comment