Mkuu wa
Mkoa wa Rukwa Mh. Joackim Wangabo amewatahadharisha watumishi
kutobweteka baada ya aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Kamishna Mstaafu
Zelote Stephen kustaafu na kumkabidhi yeye kijiti cha utekelezaji wa
shughuli za maendeleo ya mkoa.
Amesema kuwa hatomwangusha Rais
Dk. John Pombe Magufuli kwa kumuamini na kumkabidhi madaraka hayo na
kuahidi kuwa ataimarisha elimu inayoonekana bado ipo chini kwa ufaulu
lakini pia kuendeleza kasi ya uzalishaji katika kilimo.
“Baada ya
kusoma kabrasha hili la kukabidhiana ofisi kuna mambo mengi ya
kuyazingatia ikiwemo, elimu, kilimo, ulinzi na usalama, utunzaji wa
mazingira, uvuvi na uwekezaji katika viwanda. Hasa katika elimu maana
mimba ni nyingi, kuna upungufu wa madawati, upungufu wa vyumba vya
madarasa lakini pia kiwango cha ufaulu hakijafikia kile kilichopo katika
ilani ya Chama cha Mapinduzi ambayo ni asilimia 80 kwa darasa la saba,”
Alisisitiza.
Mh. Wangabo ameyasema hayo katika makabidhiano ya
ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Rukwa mapema leo hii tarehe 31/10/2017 katika
ukumbi wa ofisi hiyo, jambo lililoshuhudiwa na watumishi wa sekretariet
ya Mkoa pamoja na baadha ya Halamashauri.
Katika kuhakikisha
utendaji kazi unakuwa wa ufanisi Mh. Wangabo amesema kuwa hupemda
kusikiliza mipango ya watendaji inayotekelezeka ili waweze kuitekeleza
kama walivyoipanga nay eye ataisimamia na kutoa ushauri wa kuongeza kasi
ya utekelezaji pale inapobidi ili kuyafikia malengo waliyojiwekea kwa
wakati.
Kwa upande wake aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Kamishna
Mstaafu Zelote Stephen amewashukuru watumishi wote wa serikali katika
Mkoa wa Rukwa pamoja na wananchi wa mkoa kwa kumpa ushirikiano katika
kipindi chote alichokuwepo na kuwaomba waendeleze kumpa ushirikiano huo
huo Mkuu wa Mkoa mpya ili naye aweze kufanya majukumu yake kwa ufanisi.
Mkuu wa
Mkoa wa Rukwa Mh. Joackim Leonard Wangabo (kushoto) na Mh. Zelote
Stephen (Waliokaa) katika picha ya pamoja na Kamati ya Ulinzi na Usalama
ya Mkoa, Wakuu wa Wilaya pamoja na baadhi ya Wakurugenzi wa Halmashauri
na Mwenyekiti wa CCM Mkoa.
Mkuu nwa
Mkoa wa Rukwa, Mh. Joachim Leonard Wangabo akisalimiana na Meneja wa
PS3 Mkoa wa Rukwa Bi. Rose wakati wa kumkaribisha Mh. Wangabo katika
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Rukwa tayari kwaajili ya Kuanza kazi.
Aliyekuwa
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa, Kamishna Mstaafu Zelote Stephen (kushoto)
akimkabidhi nyaraka za ofisi Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joackim Wangabo.
katika makabidhiano ya ofisi hiyo yaliyofanyika katika ukumbi wa ofisi
ya Mkuu wa Mkoa.
Aliyekuwa
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa, Kamishna Mstaafu Zelote Stephen (kushoto)
akisaini nyaraka za ofisi Mkuu wa Mkoa kwa ajili ya Kumkabidhi ofisi
hiyo Rukwa Mh. Joackim Wangabo
Pages
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment